Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 14 Desemba 2015
NAPE:NATAKA BAJETI YA WIZARA YA HABARI IONGEZWE .
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Habari inakuwa hapa nchiniWAZIRI wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Nape Nauye amesema kuwa Atahakikisha bajeti ya wizara yake inaongezwa ilikuwezesha wizara hiyo kuendana sambamba na kauli mbiu ya Rais wa jamuhuri ya muungano watanzania JONH Pombe Magufuli ya ‘’hapa kazi tu’’
.
Akizungumza Katika Hafla yamakabidhiano ya ofisi hiyo jijini Dar es salaam mapema hii leo ,Nape Nauye amesema kuwa wizara hiyo imekuwa ikibeba shughuli nyingi za kiserikali ambazo nimuhimu lakini wizara hiyo katika mchanganuo wabajeti imekuwa ikipewa kiasi kidogo cha fedha nakushindwa kukamilisha majukumu yake kwa wakati kutokana na uhaba wa fedha .
‘’Wizara hii inabajeti ndogo sana lakini inawadau wengi sana pia kunavitendea kazi vichache lakini wizara hii hatuwezi kwenda ikiwa tuna bajeti ndogo ‘’Alisema Waziri wa Habari Napenauye .
NAPE Nauye alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake kama waziri wa habari amewahaidi kushirikiana na waandhishi wa habari ikiwemo kuondoa sheria kanda mizi zinazo mzuia mwandishi wa habari kutekeleza majukumu yake.
Alisema kuwa kuhusiana utendaji wake kuwa nilazima watu watofautishe utendaji wake ndani ya chama kwani kwa katika wizara hiyo amehaidi kuwa mtendaji namtumishi wa wizara hiyo ilikuhakikisha tasnia ya habari inasonga mbele .
‘’Mimi nitakuwa mlezi badala yakuwa mtawala nitahakikisha mnakuwa nasheria nzuri zinazo waelekeza kutimiza wajibu wenu pia niwaomba nilazima waandishi wa habari mzingatie mipaka ya utoaji wa habari inayozingatia weledi ‘’Aliongeza WAZIRI Nape.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni