Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Ijumaa, 11 Desemba 2015
UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA EURO MILIONI 16.5 KUSAIDIAWAKIMBIZI.
Timothy Marko.
SERIKALI ya ujerumani imeipatia Tanzania uro milioni 16.5 iliziweze kusaidia uboreshwaji wa kambi mbalimbali za wakimbizi hapa nchini ikiwa nijuhudi za nchi hiyo kutambua mchango wa kuwahudumia wakimbizi wa kutoka nchi za DRC na Burundi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ubalozi wa ujerumani uliopo jijini Dar es salaam mapema hii leo Muwakilishi mkazi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi nchini JOYCE Mends –COLE amesema kuwa hadi kufikia mwezi april mwaka huu jumla ya wakimbizi 116000 waliweza kukimbilia nchini Tanzania wakitokea nchini Burundi kutokana hali ya kisiasa nchini humo .
‘’Jumla ya wakimbizi 64000 waliweza kupokelewa katika kipindi cha mwezi april mwaka huu wakitokea katika nchi ya Kidemokrasia ya congo hadi hivi sasa jumla ya wakimbizi 180,000 wameweza kupokelewa ambapo idadi kubwa ya wakimbizi hao wakitokea nchini BURUNDI’’Alisema JOYCE MENDS –COLE .
Mends Cole amesema kuwa kwa kutambua mzigo mkubwa ulionao nchi ya TANZANIA katika kuwa hudumia wakimbizi shirika hilo linaipongeza serikali yaujerumani kuweza kuisadiaTANZANIA kiasi hicho cha fedha ilkutatua changamoto mabalimbali kiwemo upatikanaji wa majisafi nasalama pamoja na chakula katika makambi hayo .
Katika hatua nyingine Muwakilishi wa serikali kutoka wizara ya mambo yanje Celestine Mushy amesema kuwa serikali yaTanzania inawataka wadaumbalimbali wa jumuhia ya kimataifa ikiwemo nchi tajiri kuweza kusaidia nchi ya TANZANIA illi kuweza kuondokana na mzigo mkubwa wa kuwahudumia wakimbizi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni