Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 30 Novemba 2015
JESHI LAPOLISI LAWASHIKILIA WATANO KWA WIZI WAMAKONTENA BANDARINI.
Timothy Marko
KUFUATIA agizo la waziri mkuu KASSIMU MAJALIWA lakuwataka watuhumiwa wa wizi wa mankontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na jeshi la polisi ,jeshi hilo limesema kuwa tayari lina washikiliawatuhumiwa watano katika kuhusika nasakata hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ,jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa upelelezi CP Diwani ATHUMAN amesema kuwa sambamba na ukamatwaji wawatuhumiwa hao pia jeshi hilo limesema kuwa linaendelea kuwafuatilia watuhumiwa wengine saba wanaohusika katika tuhuma hiyo.
‘’Kufuatia uchunguzi unaofanywa nawatalaam waliobobea katika uchunguzi wa makosa ya uhalifu wa kifedha wa jeshi la polisi hadi sasa watuhumiwa kumi nambili wamekamatwa wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali nipamoja na TIAGI MASAMAKI (56)kamishina wa idara ya Forodha na ushuru TRA,HABIB MPONEZIA (45)Meneja wa kitengo cha huduma TRA, ELIAICHI MREMA(31)Msima mizi wakitengo cha ushuru wa forodha , HAROUN MPANDE (27)Kitengo cha mawasiliano ya kompyuta (ICT)-TRA pamoja na Mchambuzi mwandamizi wa masuala ya biashara HAMIS OMARY (48)’’Alisema Diwan Athumani.
Mkurugenzi wa upelelezi CP DIWAN athuman alisema kuwa watuhumiwa wengine saba wanaendelea kufanyiwa uchunguzi na jeshi hilo ilikuhakikisha hatua za kisheria zinachukua mkondo wake .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni