Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatano, 12 Agosti 2015
SERIKALI:HATUNA MGONJWA WA EBOLA.
Timothy Marko.KUFUATIA kuwepo kwa taarifa ya kuingia kwa ugonjwa wa Ebola nchini,Hatimaye serikali imekanusha taarifa hizo zilizo ripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kumekuwepo namgojwa wa ugonjwa huo katika kambi yakuhifadhia wakimbizi iliyopo Nyarugusu mkoani kigoma agosti 9 mwaka huu.
kwamujibu wa taarifa iliyotolewa leo,jijini Dar es salaam, na Afisa habari wa wizara ya Afya Catherine Sungura ili eleza kuwa tukio la kupokelewa kwa mgonjwa huyo ambaye anasadikiwa kuwa naumri wa miaka (39)lilitokea katika kambi ya nyarugusu ambapo kambi hiyo hutumika katika kuwa hifadhi wa kimbizi wa nchi za jirani Ruwanda na burundi ndipo ilipo weza kubaini kuwa kulikuwepo na mgonjwa huyo ambaye alipokelewa katika hospitali ya mkoa iliyopo maweni mkoani humo .
''Mgonjwa huyu alikuwa ni mkimbizi wa nchi ya Burundi ambaye ameishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani kigoma kwazaidi ya miaka mitatu mgonjwa huyu alikuwa asafirishwe kutokana na mpango wa kawaida washirika lakudumia wakimbizi UNHCR na kwenda nchini Marekani ambapo mgojwa huyu ilkuwa asafirishwe nchini humo tarehe 9agosti mwaka huu '' ili eleza Taarifa hiyo .
Aidha taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya hapo kulikuwepo kwa hatua mbalimbali ikiwemo kufuatilia taarifa za matibabu ya mgonjwa huyo lakini Hata hivyo bado jithada zinafanyika kuwapata ndugu wa mgojwa huyo wa ugonjwa wa Ebola .
Hadi hivi sasa takwimu za ugonjwa huo zinaeleza kuwa jumla vifo 11,269 vilipatikana katika nchi za liberia,siera Leone,pamoja na Gunea ambapo kati yawagojwa 27,705 walipatikana naugonjwa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni