Timothy Marko.SERIKALI imesema kuwa itaendelea Kuzifanyia uchunguzi Sampuli za mgonjwa aliyebanika kuwa anavimelea vya ugonjwa wa Ebola uliosadikiwa kutokea katika kambi ya wakimbizi ya Nyalugusu mkoani Kigoma .
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam,katibu mkuu wa wizara ya Afya Donard Mmbando amesema kuwa wakati serikali ikindelea kufanya uchunguzi wake aliyebanika na ugonjwa huo serikali iliendelea kumfanyia matibabu bahati mbaya mauti ilimkuta mgonjwa huyo anayesadikiwa ni raia wa Burundi .
'' Serikali tunaendelea kufanya uchunguzi wakina kuhusiana namgonjwa huyu wa ebola wakati huohuo uongozi wa hospitali yakigoma unaendelea kufuatilia ndugu wakaribu wa mgojwa huyu sambamba na wahudumu wa afya walio muhudumia mgonjwa ambaye ni raia wa burundi endapo wataonesha kuwa wanadalili za ugonjwa wa ebola''Alisema Donard Mmbando .
Mmbando alisema kuwa baada yakuchukuliwa kwa sampuli hizo agosti 11 mwaka huu katika maabara ya taifa yajamii ulibaini kuwa kulikuwepo na virusi ambavyo vilionyesha kuwa na visababishi vya kutokwa na damu nyingi lakini virusi hivyo havija onesha kuwa kulikuwa na mambukizi mapya yanayo tokana na virusi hivyo .
Alisema kuwa aidha wamejaribu kuzipeleka sampuli hizo katika maabara ya nchi yajirani nchini Kenya mjini Nairobi ilkuweza kufanya uhakiki ilkuweza kulinganisha ubora wa kimaabara .
''Mazishi ya marehemu huyo yamefanyika chini ya uangalizi wa afya mkoa kwa kuzingatia taratibu wakanuni za kimataifa za kuzuia maambukizi ''Aliongeza Dk Mmbando.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni