Jumatatu, 27 Oktoba 2014

NECTA :TUMEDHIBITI VITENDO VYA UDANGANYIFU


Timothy Marko.
BARAZA la mitihani nchini (NECTA)limesema kuwa limeweza kudhi biti vitendo vya udanganyifu katika mitihani ambapo katika kipindi cha mwaka 2011/13 vitendo vyaudanganyifu katika mitihani vimeweza kupungua pindi mitihani inayoratidiwa na baraza hilo inapofanyika .
Akizungumza nawaandishi wahabari jijini mapema hii leo,Katibu mtendaji wabaraza hilo Charles Msonde amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana watahiniwa waliofutiwa matokeo walikuwa 13 ikilinganishwa watahiniwa 9,736waliobanika kufanya vitendo vya udaganyifu 2011/12 ni 293 tu walibainika kufanya vitendo hivyo.
‘’Aidha katika mtihani wakidato cha nne mwaka jana watahiniwa walio futiwa matokeo kutokana navitendo vya udanyifu walikuwa 13idadi ambayo nindogo ikilinganishwa watahiniwa 9,736waliobanika kufanya vitendo hivyo mwaka 2011/12 watahiniwa 293’’.alisema Charles Msonde.
Msonde alisema kuwa katika mtihani wakidato cha nne mwaka jana jumla yawatahiniwa walifutiwa matokeo yao kutokana navitendo hivyo vya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa nawatahiniwa 789 kwa mwaka 2012 ambapo jumla yawatahiniwa 3,303kwa mwaka 2011.
Katika hatua nyingine Katibu mtendaji wa baraza hilo Charles Msonde alisema kuwa baraza hilo limeweza kuendana nakasi ya sayansi na tenknolojiakwakufanya usahili wa watahiniwa kwakutumia Tehama ambapo watahiniwa hutegemea kufanya usahili katika wavuti ya baraza hilo .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni