Jumatano, 10 Septemba 2014

UNDP YAISAIDIA TANZANIA KATIKA KUBORESHA UCHAGUZI

Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha kuwa Demokrasia inakuwa kwakiwango kikubwa hapa nchini Shilirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP)limetoa msaada wa kompyuta zenye jumla ya dola lakimbili nanusu (250,00000)ambazo nisawa shilingi milioni sita  kwafedha yakitanzinia ilkuweza kusaidia uchaguzi unaotajiwa kufanyika mwakani .

Akizungumza jijini leo hii, Muwakilishi mkaazi Shilika la maendeleo la umoja wa mataifa  Philippe Poinsot amesema kuwa msaada huo umekuja ilikuhakikisha uchaguzi unaotajia kufanyika mwakani unakuwa huru na wahaki na wenye tija kwa taifa .

‘’Msaada huu wa kompyuta kwa tume ya uchaguzi unao gharimu shilingi milioni sita ambao nisawa nadola laki mbili nanusu umekuja ilkuhakikisha demokrasia nchini inakuwa ambapo kiini chake ni uchaguzi huru na wahaki ‘’Alisema Philippe Poinsot.

Poinsot alisema kuwa msaada huo umelenga katika kuleta matokeo kwa uharaka pale inapobidi matokeo hayo kuwa na ulazima .
Kwaupande wake Msajili wa vyama vyasisa Jaji Franciss Mtungi amesema kuwa kutokana na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 umoja wa mataifa unafanyajitihada za kuhakikisha ucha guzi unakuwa huru nawahaki .

JAJI Franciss amesema kuwa tekenolojia ya mawasiliano inayo mchango mkubwa katika kuimarisha demokrasia ikiwemo matumizi ya vifaa hivyo katika uchaguzi .

Alisema kuwa msaada huo utawezesha ofisi ya msajili wa vyama vyasiasa kuweza kukusanya takwimu kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa ikiwemo kufanya uhakiki wa vyama vyasiasa .
‘’kiukweli dunia yaleo unapokokuwa namasiliano hafifu una pokea matokeo hafifu ‘’Alisema jaji mtungi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni