Jumatano, 6 Agosti 2014

MAKAMPUNI MAWILI YABAINIKA KUUZA VILAINISHI FEKI VYA MAGARI.


Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi zinakuwa naubora unaotakiwa ofisi ya mkemia mkuu waserikali imebaini uagizwaji wa vilanishi feki visivyo naubora vilivyo chini ya kiwango ambavyo vimeanishwa na ofisi hiyo .

Utafiti huo uliofanywa naofisi ya mkemia mkuu ulibainikuwa katika kipindi cha mwezi septemba mwaka jana hadi January mwaka huu kumekuwa na baadhi ya makampuni mawili yaliingiza vilainishi hafifu vilivyo chini yakiwango ya asilimia sabini nanane na tisini namoja na kueleza kuwa ni kampuni moja tu ambayo ilikidhi vigezo vilivyo wekwa na serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo,Mkemia mkuu wa serikali profesa Samweli Manyele amesema kuwa baadhi yamakampuni yaliyo kamatwa ambayo yamehifadhiwa kwasababu maalum za kiuchunguzi yalingiza bidhaa zisizokuwa naubora .

‘’Katika kipindi cha mwezi februari hadi julai mwaka huu jumla ya sampuli 114 zilichukuliwa na wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali yanaonesha kuingiza nchini kwa malighafi yavilainishi vyenye ubora unaokubalika ‘’Alisema Samweli Manyele .
Profesa Samweli Manyele alisema halihiyo inatokana uchukuaji wa sampuli umekuwa ukifanywa na wenye mizigo nakuchukuliwa sampuli kufuatia maagizo yaliyo tolewa na ofisi yamkemia mkuu uliagiza kuwa lazima uchukuaji wasampuli lazima uchukuliwe kitalamu ilkuweza kuleta matokeo bora ya uchunguzi.

‘’Kutokana nauchunguzi huu ofisi yamkemia mkuu wa serikali imebaini madhara yakuwepo kwauuzwaji wa vilaishi feki nipamoja nakuharibika kwa mitambo nainjini za magari napamoja nakuongezeka kwa gharama za matengenezo ya magari ‘’Aliongeza Mkemia mkuu Samweli manyere .
Katika hatua nyingine Mkemia mkuu wa serikali amwewataka mawakala wanaoagiza vilainishi kufuata kanuni zilizowekwa kisheria ambazo zinamtaka kila wakala awakilishe nakala husika pindi wanapo ingiza bidhaa nchini kama vile ‘’billof landing’’ilikusaidia utambuzi wa mizigo inayotoka kila nchi husika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni