Timothy Marko.
Katika kuhakikisha sekta ya elimu ya juu inakuwahapa nchini serikali kwa kushirikiana na tume ya vyuo vikuu Tanzania imeainisha viwango vya gharama vya ada katika ngazi mbalimbali ikiwemo ngazi ya awali ,kati pamoja naile yajuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, kaimukatibu wa tume ya vyuo vikuu nchini Magishi Mgasa amesema kuwa tangu kipindi cha mwaka 2000 serikali imekuwa katika jitihada za kutafuta mfumo bora wa kubainisha na kupanga viwango vya ada za masomo ya elimu ya juu.
‘’Tangu mwaka 2000 serikali imekuwa katika jithada za kutafuta mfumo bora wa kubainisha na kupanga viwango vya ada za msomo kwa ngazi yaelimu yajuu’’alisema Magishi Mgasa.
Magishi Mgasha alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/12 serikali kupitia ufadhili wa benki ya dunia katika mradi wa sanyansi na tenknolojia chini ya wizara ya sayansi imeweza kuajiri mtaalamu mshauri ilikuweza kufanya utafiti kuhusiana na gharama za msomo katika vyuo vikuu mbalimbali.
Alisema kuwa katika matokeo yaliyofanywa kuhusiana na gharama za mafunzo zinazotolewa navyuo hivyo serikali iliweza kufanya upembuzi akinifu ilikuweza kuandaa mfumo bora utakawezesha kutambua gharama za masomo yajuu.
‘’Napenda ifahamike kuwa mfumo huu tunao uzungumzia leo hii umeteng’enezwa na wataalamu wetu watanzania kwa kutumia ripoti za watalamu za utafiti wa awali kwa kukusanya taarifa za gharama halisi za ada kwa program za masomo zinazofundishwa hapa nchini katika vyuo binafsi na vile vya serikali’’aliongeza Mgasha .
Mgasha aliongeza kuwa katika taasisi zinazoshughulika naubora wa elimu hapa nchini ikiwemo Tume yake na baraza la elimu ya ufundi (Nacte)sambamba na Baraza la mtihani (Necta)pamoja na wadau wengine waelimu umeweza kuandaa mfumo wa elimu wa kuwashirikisha wadau hao katika sekta elimu nchini.
Aliongeza kuwa ,vyuo vyabinafsi pamoja navile vya umma vilitembelewa nakuhusishwa katika utoaji wa takwimu halisi za gharama wanazotumia katika uendeshwaji wa masomo.
‘’Mchakato wauandaaji wamfumo huu ulikuwa shirikishi na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wavyuo vikuu ,taasisi za mamlaka wa udhibiti wa elimu wanafunzi wa elimu yajuu na wadau wengine ‘’aliongeza Mgishi Mgasha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni