Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi habari kuhusu sakata la wanafunzi hewa Jijini Dar es Salaam |
Timothy Marko
Kufuatia kuwepo kwa
sintofahamu ya malipo hewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini, Serikali
imewataka wakuu wa vyuo vikuu hapa nchini kuhakikisha wanafunzi waliochukua
mikopo hiyo ambao hawakuwa na sifa stahiki kufanya marejesho ya mikopo
hiyobaada ya siku saba.
Akizungumza na
wahandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa vyuo vya elimu vinatakiwa kuweka mfumo
mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili na matokeo ya
majaribio ya mitihani sambamba na akaunti
za benki ambazo mikopo hiyo ililipwa.
“Bodi ya Mikopo
inapaswa kuchambua na kuingiza mara mabadiliko ya taarifa za wanafunzi kama
ilivyo pelekwa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasio
stahili, hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wotevwaliohusika kufaniksha
malipo kwa wanafunzi ambao hawapo vyuoni” Alisema Ndalichako
Waziri Ndalichako
amesema ukaguzi huo utahusisha wafanyakazi wa bodi ya mikopo na vyuo husika pia
amevitaka vyuo viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa wanufaika wa
mikopo ili kuepuka kufanya malipo ya wanafunzi hewa.
Pia Waziri Ndalichako
ameeleza kuwa Wakuu wa vyuo waweke mifumo ya uhakiki wa usahili wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa
bodi ya mikopo, ambapo amesisitiza kuwa bodi ya mikopo watawajibika kwa usahili
wa zoezi hilo kwani hivi karibuni kumebaini ka kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo
ya wanafunzi ambao hawakufnaya mtihani na wamefeli na wameandikiwa kuwa
wamefaulu (PASS) ili waendelee kupata mikopo hiyo.
“Uchunguzi zaidi
utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambazo zimelipwa kwa
watu wasio stahili hatua hii inatokana na matokeo ya uchunguzi ambao umebaini
kuwepo kwa bbadhi ya wanafunzi waliohitimu tangu mwaka 2013 lakini wameendelea
kupokea fedha na wengine wamefukuzwa kwa kushindwa masomo tangu mwaka 2013-2014
lakini bado wameendelea kulipwa hadi mwaka 2015-2016”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni