Jumatano, 24 Agosti 2016

JESHI LAPOLISI KUANZISHA MSAKO WA WATUHUMIWA WAMAUAJI YA ASKARI POLISI JIJINI.

Tokeo la picha la nsato mssanzya
.
Kamishina Operesheni na Mafunzo CP Nsato Marijani Mssanzya .

 Timothy Marko .

KUFUATIA kuwepo kwa taarifa za kuuwawa Askari wa jeshi lapolisi wanne huko mbagala maeneo ya Mbande jana saa moja usiku , Jeshi lapolisi nchini limesema kuwa linaendelea nauchunguzi ilikuweza kuwabaini wahalifu walio husika natukio hilo .

Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es salaam Kamishina Operesheni na Mafunzo CP Nsato Marijani Mssanzya aliwataja askari hao waliofariki katika tukio hilo ni E.5761 CPL Yahaya F.4660CPL Hatibu ,G.9524 PC TITO pamoja na PC Gastone .

''Wengine ambao ni Raia walijeruhiwa katika tukio hilo nipamoja Ally Chiponda ,Aziz Yahaya ambao wote ni wakaazi wa eneo la Mbande ,katika tukio hilo majambazi hayo yalifanikiwa kupora silaha mbili aina yaSMG na Risasi Sitini ,hakuna pesa wala au mali yabenki iliyoharibiwa  nidhairi wahalifu hawa walikuwa na kusudio moja tu lakuwashambulia askari polisi ''Alisema Kamishina Operesheni na mafunzo Nsato  Mssanzya .

Kamishina Mssanzya alisema kuwa baada yatukio hilo kulikuwa nabaadhi watu waliondika taarifa za kubeza nakukejeli mazoezi yakawaida yanayofanywa najeshi lapolisi ambapo wengine waliandika ujumbe wa kushabikia tukio hilo la kuuwawa kwa askari polisi hao .
Alisema kuwa watuhumiwa hao waliandika ujumbe unaowadhihaki jeshi hilo nakuwataka askari hao kutoka uraiani na kuwataka askari hao kukaa kambini .

'' Katika tukio hili lakushambuliwa kwa askari polisi kumekuwa na baadhi ya viongozi wasiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakiwahamasisha wafuasi wao wawa shambulie askari polisi ''Aliongeza Nsato.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni