MWENYEKITI wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) Martin Munisi |
Timothy Mark.
MWENYEKITI wa
umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) Martin Munisi wa wilaya ya Arusha mjini ameliomba jeshi la polisi kumkamata mara moja
mbunge wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha Chadema Godbless Lema kwa
kitendo chake cha kumkashifu na kumtamkia Rais Magufuli kuwa atapoteza uhai
kabla ya 2020!.
Mwenyekiti huyo
Martin Munisi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza na kituo kimoja
cha redio kilichopo jijini humo, huku mbunge huyo akisisitiza kama
hatawasikiliza chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)
Katika hatua nyingine Munisi amelitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi wa
mikutano iliyokatazwa na inayotakiwa mbunge huyo anafanya mikutano ya
chama chake na siyo mikutano ya mbunge kama inavyofahamika na ambayo
inatofautiana na ahadi za mbunge kwa wananchi kupitia chama chake.
Mikutano ya
mbunge hulenga kuzungumzia ahadi za mbunge alizotekeleza, atakazotekeleza na
kuhamasisha maendeleo ila kinyume chake Lema yeye anasema wananchi wataingia
barabarani maana hali ni mbaya mara raisi takufa kabla ya 2020
“haya ni maneno yasiyovumilika hata kidogo kwenye jamii iliyostaharabika ni vizuri jeshi letu likamhoji mbunge lema kuhusu kumzushia au kutabiri kifo kwa mwenyekiti wetu wa chama, taifa na Rais wetu, kwa vile Lema hana agenda na nalitaka jeshi la polisi kuzuia mikutano yake kama wasipozuia sidhani kama vijana wa ccm na wananchi wapenda nchi yao watakuwa tayari kuvumilia matusi ya lema kwa mh Rais, wetu mpendwa” alisema Martin Munisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni