Jumatano, 21 Septemba 2016

TAASISI YA SOCIETYA WATCH YAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA WATOTO YATIMA.

Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha watoto yatima hawaachwi nyuma katika suala zima la elimu nchini ,Taasisi ya Society Watch imeanzisha kampeni maalum kundi hilo kutokana na watotot yatima kuwa  changamoto mbalimbali zinazofanya ndoto zao zishindwe kutimia.
 Akizungumza na waandishi wa habari  jijini  Dar es salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Society Watch, Simon Mnkondya wakati wa kukabidhi cheti utambuzi wa kazi ya msanii Kallah Jeremiah kushirikisha watoto katika wimbo wana  ndoto, amesema kuwa watoto yatima wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo kunahitaji jitihada za kuweza kusaidia watoto yatima.
 Mkondya amesema kuwa mpango wa utaoji wa elimu kwa serikali kwa kundi hilo inawezekana kutokana na  uchache.

Amesema kuwa watoto yatima wamepata hamasa kwa  wimbo wa Mwanamziki wakikizazi kipya Kala jeremiah ''wanandoto'' ambapo taasisi hiyo imeliona kundi hilo linalo umuhimu wakipekee yakutoachwa nyuma katika suala la kupata elimu .

''Hamasa ya taasisi yetu Society Watch nikuwasaidia watoto yatima walipo vijijini katika kupata elimu hasa kwa watoto wanaishi katikamazingira magumu katikamaeneo yavijijini ,hamasa hii imetokana na wimbo wa wanandoto wakala jeremamiah kwani watoto hawa wanao mchango mkubwa katika kulitumikia taifa ''Alisema Mkurugenzi Simon Mkondya.



Amesema kuwa kutokana na msanii huyo wakizazi kipya Kala jeremiah  kuona umuhimu watoto yatima kupewa fusra yakupata elimu kama watoto wengine kupitia wimbo wanandoto unalenga kuihamasisha jamii kulisaidia kundi hilo maalum katika kupata elimu 
.
Mkondya amesema serikali inaowajibu wakipekee katika kuwasaidia watoto yatima kuwawezesha kundi hilo kuweza kupata elimu kwani kutokana naumuhimu wawatoto hao katika kujenga taifa nakuliletea taifa maendeleo katika hazina yaviongozi wakesho ,hivyo serikali najamii inawajibu wakulisaidia kundi hilo katika kuwapatiaelimu.

Nae  Msanii wa kizazi kipya nchini Kallah Jeremiah amesema kuwa yeye pamoja nawanamziki wa kizazikipya wameimba wimbo huo''wanandoto'' kuikumbusha serikali kuwaasaidia watoto yatima walipo katika mazingira magumu kuwa wanao umuhimu wakipekee katika kupata elimu .
Amesema kuwa ni mara kwanza kwa watu kumpa cheti kwa kukubali kazi anayoifanya katika jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni