MWENYEKITI WA PAROLE AGUSTINO MREMA. |
Timothy Marko .
MWENYEKITI wa bodi Parole nchini ,Agustino Mrema amesema atakwenda kwa Rais wajamuhuri
wa Muungano wa Tanzania Dk.Jonh Pombe Magufuli kumpelekea Mapendekezo ya
Wafungwa walio namakosa madogo yasiyo ya jinai kuweza kupewa kifungo cha nje
,ilikuweza kuhakikisha wafungwa hao wanalitumikia taifa ikiwemo uteng’enezaji wa
madawati .
Akizungumza Katika Kikao cha Bodi hiyo katika
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza nchini jijini Dar es salaam Agustino Mrema
amesema kuwa wafungwa walio kuwa namakosa madogomadogo ambayo sio ya jinai wanatakiwa
kusimamiwa vizuri kwani wafungwa hao endapo watasima maiwa wataliwezesha taifa
kuondokana na tatizo la uhaba wa madawati nakuondokana tatizo la uhaba wa
madawati .
‘’Solution sio kufunga watu miaka mingi lakini
tunatakiwa kuwa simamia vizuri tukiwadhibiti wafungwa hawa wanaweza kujenga
taifa ,nilazima tuweze kuwafikiria hawa watu ‘’Alisema Agustino Mrema .
Mrema alisema kuwa sambamba na kuwapatia kifungo
chanje wafungwa waliopo magerezani pia alimuomba Rais Magufuli kuweza kuwapatia
vitendea kazi Jeshi la Magereza ilikuweza kutenda kazi zao kwa ufanisi .
Alisema kuwa endapo jeshi hilo lisipopewa vitendea
kazi kazi ya kuwa hudumia wafungwa itakuwa ngumu nahivyo kuweza kusababisha
jeshi hilo kushawishika katika vitendo vya rushwa vinakavyo wachochea Baadhi ya
wafungwa kuweza kutoroka Magerezani .
‘’Kuna mambo lazima tuwafikirie hawa watu
wanafanya kazi kubwa kwani wana kumbana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu
wavitendea kazi ikiwemo magari hii lazima nitaipeleka kwa mheshimiwa Rais ili
aweze kuwasaidia ‘’ Aliongeza Mrema .
Kwa upande Wake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini
Jonh Minja amesema kuwa kumekuwa nachangamoto kubwa kwa wananchi juu ya uelewa
wa haki za wa fungwa magerezani ikiwemo haki za mfungwa kupewa kifungo cha nje
.
Alisema Wananchi wengi wamekuwa nadhana potofu juu
yamfungwa kupewa kifungo cha nje ya magereza kuwa anaweza kuleta madhara
makubwa kwa jamii .
‘’Nilazima elimu itolewe kwa jamii hasa kupitia
vyombo vya habari juu ya hakimbalimbali za mfungwa kuweza kupewa kifungo cha
nje ya magereza hasa kwa wafungwa wasikuwa na makosa yakihalifu kwa jamii’’Alisema
Kamishina Jonh MINJA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni