waziri waelimu namafunzo yaufundi Profesa JOYCE NDALICHAKO. |
Timothy
Marko.
SERIKALI
imesema kuwa katika kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa natija hapa nchini
itaendelea kushirikiana nawadau mbalimbali wasekta hiyo ikiwemo jamii ili kuwezesha
mpango wezeshi unaolenga kukuza kiwango cha ubora wasekta hiyo .
Akizungumza
katika kongamano la uzinduzi wa ripoti ya ubora waelimu unaolenga kutathimini
Kusoma kuandika na kuhesabu Waziri wa Elimu na mafunzo yaufundi Profesa Joyce
Ndalichako amesema kuwa ilikuwezesha mpango wa uboreshwaji wa sekta ya elimu
nilazima wadau mbalimbali wakiwemo wazazi walimu watunga mitaala yaelimu kuweza
kushirikiana katika kuwezesha mpango wa KKK una tekelezwa kwa vitendo .
‘’Tunahitaji
matokeo bora katika kuhakikisha mpango huu wa KKK yani kusoma kuandika
nakuhesabu unatekelezwa kwa vitendo kama
hatutashirikiana na wadau mbalimbali wasekta yaelimu KKK hazitoweza kukamilika ‘’Alisema
Profesa Joyce Ndalichako .
Waziri wa
elimu na mafunzo yaufundi profesa Ndalichako alisema kuwa katika kuwezesha
mpango huo wa kujua kusoma kuhesabu na kuandika unatekelezwa serikali
itashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau mbalimbali wa mandeleo ikiwemo
shirika la USAID ilikuweza kuhakikisha mpango huo wa ubora waelimu wa kujua
kusoma kuhesabu nakuandika unatekelezwa .
‘’Katika
kulifanikisha hili la ubora waelimu naiomba jamii isiachwe nyuma katika
kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuweka mipango mikakati ya kuboresha sekta ya
elimu ikiwemo kuboresha mazingira wezeshi ya zana zakufundishia ikiwemo
madarasa vitabu pamoja na ubora wa walimu ‘’Aliongeza Waziri waelimu na mafunzo
yaufundi profesa Joyce Ndalichako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni