Jumatano, 4 Mei 2016

SERIKALI YATAKIWA KUANGALIA UBORA WA WAKUNGA WANAOTOA HUDUMA KWA WANAWAKE.

Timothy Marko.

SERIKALI imetakiwa kuangalia upya ubora wa wakunga nchini kwa lengo la  kuondokana na vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi.

Tokeo la picha la NEMBO YA CHAMA CHA WAKUNGA TANZANIA
SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOJIHUSISHA NAIDADI YAWATU.

Wito huo umetolewa na mwakilishi mkazi wa shirika la umoja wa mataifa(UNPA) Julita Onabanjo linaloshughulikia  idadi ya watu amesema kuwa, tanzania imepiga hatua kubwa kuondokana na vifo vitokanavyo na uzazi kwa wanawake .

 

"Suala la wakunga kuhudumia jamii sio wingi wao bali idadi hiyo ya wakunga iendane na ubora wawakunga wanaozalishwa  katika vyuo mbalimbali vya afya ili kuweza kuondokana na wakunga wasiokuwa na ujuzi"alisema Julita.

 

Julita alisema kuwa tanzania imekuwa ni kinara mkubwa katika kupunguza vifo vya wananawake na watoto vitokanavyo na uzazi ,hata hivyo shirika hili kwa kushirirkiana na tanzania imeweza kupiga hatua kubwa katika kuhakikisha tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi vinapungua.

 

Aidha takwimu zinaonyesha kumekuwa na vifo zaidi ya 400 kila mwaka vitokanavyo na masuala ya uzazi suala hili limekuwa ni ajenda ya kimaifa ambapo inaonyeshwa kuwa limechangiwa na ukosefu wa wakunga wasio kuwa na ujuzi wa kutosha.

 

Kwa upande wake Rais wa chama cha wakunga nchini Fedy Mwanga  amesema kuwa,ni lazima serikali pamoja na wadau mbalimbali kupiga vita suala la ukeketaji ili kuondokanana na vifo vya uzazi kwa wanawake.

 

"Wakunga wa jadi wanatakiwa kuhamasishwa kuachana na mila potofu zitokanazo na ukeketaji kwa lengo  la kupunguza vifo vya watoto na wanawake"alisema Mwanga.

Mwanga aliwataka wakunga hao kuongeza ujuzi zaidi katika sekta yao ili waweze kutoa huduma kwa wanawake na watoto wakiwa na ubora wa hali ya juu.

Pia mwanga aliwataka kuondokana na mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wanawake na watoto kwa lengo la  kuondoa matabaka miongoni wa wazazi na watoto.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni