Ijumaa, 20 Mei 2016

MKAZI DAR ASHIKILIWA NA JESHI LAPOLISI KWAKUUZA DHAHABU BANDIA

Tokeo la picha la KAMISHINA SIRRO

KAMISHINA KANDA MAALUM SIMONI SIRRO



Timothy Marko .
JESHI la polisi kanda Maalum jijini Dar es salaam linamshikilia Weneslaus Mtui (46)mkaazi wa Makongo juu kwa tuhuma za kuuza madini Bandia .

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina wa polisi jijini Dar es salaam Simon Sirro amesema tukio hilo liltokea March14 mwaka huu majira ya saa 12:45 katika kituo cha polisi  Ostabey .

‘’Mtuhumiwa huyo alikamatwa ambayejina lake tunalihifadhi baada yakushawishika kununua Madini aina ya gold kg20 yenye thamani ya Dolla za kimarekani 40,000 sawa fedha za kitanzania milioni 90 kwa kampuni CROWN LOGISTCS  AND HANDLING ya Dar es salaam kwa ajili yakuuza nchini Italia’’Alisema Kamishina Sirro .

Kamishina Simoni Sirro alisema kuwa mlalamikaji huyo alilipa fedha hizo katika benki ya CRDB nakisha kukabidhiwa vipande vitatu vinavyosadikiwa kuwa nimadini vikiwa nakilogramu 212 nakugundulika vipandehivyo si halisi .

Alisema Baada ya jeshi hilo kufanya upekuzi kwamfanyabishara huyo ambaye aliuza vipande vya madini visivyo halisia lilibaini kuwa mtughumiwa huyo alikuwa na vitu vinavyosadikiwa kuwa nimaadini ,mashine zakupimia madini vifaa vyakubania ,mashine yakupimia madini pamoja naslip mbalimbali za benki.

Katika hatua nyingine jeshi hilo may 13 mwaka huu  limefanikiwa kukamata silaha aina yabastola yenye namba zausajili A.O8416zikiwa narisasitatu huko mbezi mwisho .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni