Jumatano, 27 Aprili 2016

NSSF KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAAJIRI WASIO PELEKA MICHANGO YA WAFANYAKAZI WAO .


Tokeo la picha la nssf


Timothy Marko.
SHIRIKA lahifadhi yajamii NSSF limesema litawachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawa rejeshi michango ya wafanyakazi wao kwawakati katika mfuko huo wa hifadhi ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa shilirika hilo Mseli Abdallah amesema zoezi lakuwafikisha waajiri wasiopeleka michango kutoka kwa wafanyakazi wao mahakamani litanza Mei mwaka huu .

‘’Michango ambayo inyotakiwa kulipwa ni asimilia 20 yamshara wa mwezi baada yamakato kutoka katika Mshahara wa mfanyakazi wake asilimia 10 ili ifike asilimia 20 nakuwasilisha kwenye shirika ‘’alisema Kaimu MKURUGENZI Mseli Abdallah.

Kaimu Mseli Abdalah alisema kuwa kitendo cha kutorejesha michango hiyo nikosa kisheria nanikosa la jinai kwamujibu wakifungu cha72(d)cha Nssf ambapo adhabu yake nipamoja nakifungo chajela miaka miwili .

Alisema aidha kitendo hicho cha kutowasilisha michango hiyo kwa wakati huwasababishia usumbufu mkubwa pindi wanachama wanapo staafu kazi .  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni