Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 21 Desemba 2015
OFISI YA MKEMIA MKUU YAPATA ITHIBATI YA KUPIMA SAMPULI ZA DAWA KIMATAIFA.
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha Bidhaa zinazotokana na Dawa zinakuwa naubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa kimataifa Mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali imeweza kupata ithibati yakimataifa ya utoaji wa ripoti za ubora wa chakula Dawa zinazowesha ripoti hizo kutumika katika upimaji wa ubora wadawa za binadamu kimataifa .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Mkemia mkuu wa serikali Samweli Manyere amesema kuwa upatikanaji huo wa ithibati kimataifa utawezesha taasisi hiyo kupima sampuli mbalimbali katika maabara zilizopo katika ofisi hiyo ilikuweza kudhibiti dawa sizizokuwa naubora kwa mtumiaji .
‘’WAKALA ime weza kupata ithibati ya ubora wa mifumo ya kimataifa 1SO 9001:2008 Ithibati hii inahusisha huduma za msingi zitolewazo nawakala ambazo ni uchunguzi wa maabara na usimamizi wa sheria ‘’Alisema Profesa Samweli Manyere .
Profesa Manyere alisema kuwa sambamba kupewa ithibati hiyo kimataifa pia taasisi hiyo imepata ithibati yauchunguzi wa sampuli kimaabara ambayo ni 17025 :2005ambayo ita wezesha taasisi za binafsi nazile za umma kuweza kuboresha bidhaa zake nakutoa huduma bora za dawa kwa umma .
Mtalaamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Daus Mgasa amesema kuwa uzinduzi naupatikaji wa ithibibati hiyo utawezesha vyombo vya usalama navile vyauchunguzi wa makosa ya jinai kuweza kuchunguza makosa mbalimbali yajinai kwakutumia mashine ili kuweza kupima sampuli ilikuweza kupata ushahidi nakuhakikisha haki inatendeka .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni