Jumatatu, 21 Desemba 2015

NAIBU WAZIRI MANYANYA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Timothy Marko. SERIKALI imewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri na manispaa zote nchini, kufwatilia kwa ukaribu utekelezaji wa utoaji wa elimu pasipo malipo kwa ngazi za shule za msingi hadi sekondari . Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Naibu waziri wa elimu ,sayansi,Teknolojia na ufundi Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa utekelezaji wa maagizo hayo unatokana na waraka uliotolewa na wizara hiyo namba 5 na 6 wa mwaka huu ambao uliwataka wakuu hao kufuatilia kwa ukaribu zaidi juu ya utelezaji wa sera ya elimu ya utoaji wa elimu bure katika ngazi ya msingi pamoja na sekondari. ‘’Napenda kusisitiza kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halma shauri za wilaya ,miji na manispaa zote nchini wafwatilie kwa ukaribu maagizo hayo ,aidha walimu watakaokwenda kinyume na maagizo hayo wata chukuliwa hatua za kisheria ‘’Alisema Naibu Waziri huyo. Mhandisi Stella Manyanya alisema kuwa jamii isisite kutoa taarifa katika ofisi za elimu za kata pamoja na makao makuu ya wizara hiyo kwa shule yoyote itakayoonekana kukiuka maaagizo hayo. Aliongeza kuwa kuhusiana na utoaji mikopo kwa elimu ya juu serikali itaendelea kutoa mikopo kwa wale wote wanaotoka katika familia masikini pamoja na yatima waliotimiza vigezo vya kupatiwa mikopo huku akisisitiza kuwa wanafunzi waliopatiwa mikopo kuitumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyo kusudiwa . ‘’Ninapenda kusisitiza kwamba wanafunzi walikidhi vigezo vya kupatiwa mikopo waitumie mikopo vizuri iliiweze kuleta tija kwao wenyewe na familia kwa kuweza kuchangia maendeleo ya nchi ‘’Aliongeza Naibu waziri Manyanya . Ikumbukwe kuwa Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Magufuli alitoa tamko kuwa kuanzia mwaka wa masomo 2016 elimu itatolewa bure bila malipo kwa shule zote za umma nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni