Jumatatu, 2 Novemba 2015

MAUZO YA HISA NDANI YA NCHI NA NJE YA NCHI YAATHIRI KIWANGO CHA HISA DSE .

Timothy Marko. KIWANGO cha mauzo ya Hisa kimeweza kushuka kutoka shilingi bilioni50 hadi kufikia shilingi bilioni 28 wakati idadi yamtaji imefikia trioni 21 Baada ya iliyokuwa Benki ya Kibishara kuongeza bei katika hisa zake kwa asilimia 3.20.
Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Biashara na mauzo wa soko hilo la hisa jijini hapa (DSE)Patrick Mmsusa amesema kuwa kushuka kwa mauzo katika kaunti hiyo ya CRDB kumetokana na kushuka kwa sekta yaviwanda kwa asilimia 48 ikilinganishwa na awali .
''kiwango cha mauzo hisa kimeshuka kutoka shilingi Bilioni 50 hadi kufikia bilioni 28 kwa wiki hii ambapo sekta yaviwanda imeweza kushuka kwa asilimia 48 na wakati huo huo makapuni yanaoyoongoza kwa ununuzi wa hisa nipamoja na TBL,asilimia (81) CRDB (12) NMB (3)''alisema Patrick Mumsusa .
Mumsusa alisema kuwa kiwango hicho kimetokana nashughuli za masoko katika soko hilo kuongezeka nakuweza kuchangia wanunuzi wa hisa wa kutoka nje na ndani ya nchi
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni