Jumatano, 28 Oktoba 2015

CCM :HATUJARIDHISHWA NA MWENENDO WA UJUMLISHWAJI WAMATOKEO YA UBUNGE .

Timothy Marko. CHAMA cha Mapinduzi (CCM)kimesema kuwa hakijaridhishwa na namna ya ujumlishwaji wa matokeo ya ubunge katika uchaguzi mkuu uliofanyika October 25 mwaka huu nakupelekea wa bunge wa upinzani kupata ushindi .
Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa kampeni wa chama hicho January Makamba amesema kuwa majimbo ambayo chama hicho hakijaridhishwa na matokeo ya ubunge nipamoja na jimbo la iringa Mjini,Mikumi,Ndanda pamoja nakawe ambapo wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo hayo walivuruga uchaguzi wakati wakujumlisha matokeo .
''Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi kutokana na utata wa ujumlishaji kura ,CCM iliomba kura zihesabiwe kwa upya lakini ikanyimwa haki hiyo yamsingi ambayo ipo kwenye sheria ikiwemo jimbo la nyamaganya ''Alisema Januari Makamba .
Januari Makamba alisema kuwa katika baadhi yamajimbo hususani Jimbo la Nyamagana vyama vyaupinzani viliweza kupewa haki yakusabiwa kwaupya nakusisitiza kuwa chama hicho kimefungua shauri mahakamani ilkuweza kupinga matokeo yamajimbo hayo
.
alisema kuwa chama chake kinataka kujiridhisha namatokeo hayo nakupima je utashi wa wananchi umeheshimiwanakusistiza bado chama hicho kinaendeleakukusanya taarifa juu yamajimbo mengine kama chama hicho kimehujumiwa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni