Jumatatu, 24 Agosti 2015

JKT YAZINDUA ZANA ZA KUKUZA KILIMO CHENYE TIJA KWA MKULIMA.

Timothy Marko. KATIKA kuhakikisha sekta ya teknolojia inakuwa hapa nchini nakuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo Wizara ya Ulinzi na jeshi lakujenga taifa imegundua mtambo maalum utakao wawezesha wakulima nchini kuwa nakilimo chenye tija.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo mkoani pwani Mkurugenzi wa kiwanda cha Nyumbu kilichopo katika mkoa huo Brigadia Jenerali Anslen Bahati amesema kuwa wakulima wanaweza kutumia mashine mbalimbali ikiwemo power tila zinazozalishwa na jeshi hilo ili kuweza kupata mazao ya uhakika kwa kipindi kifupi
.
''Mtambo huu ambao wakulima wanaweza kukuza kilimo chao nakupata mazao mengi hauuzwi kwa beighali ila unauzwa milioni kumi natano tu ambapo mkulima anaweza kulima nakujipatia mazao yake kwa muda wasiku nne tu ''Alisema Brigadia Jenerali Anslen Bahati .
Brigadia Jeneral BAHATI alisema kuwa mtambo huo utawezesha wakulima wadogo wadogo katika kuboresha hali yamazao nakukuza tija na hatimaye kujipatia kipato kitakacho wakwamua katika hali yaumasikini .
Alisema kuwa pamoja na mtambo huo kuwa nufaisha wakulima,pia kiwanda hicho kimegundua mashine mbalimbali zakuzalisha umeme kwa kutumia mfumo wa gesi ambapo mtambo huo unauwezo wakuzalisha MW 1 .
''Kwakushirikiana nachuo kikuu cha Dar es salaam tumeweza kuzindua mtambo wakuzalisha gesi ,sambamba namtambo huu pia tumegungua pamp za maji ambazo kwasiku zahivi karibuni zimekuwa zikitumiwa na shirika la kusambaza maji katika mkoa wa Dar es salaam ''Aliongeza Bahati .
Brigadia Jenerali BAHATI aliongeza kuwa pia Kitengo hicho cha Nyumbu kimekuwa kikijishughulisha namasuala mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti mbalimbali katika sekta ya usafirishaji. .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni