Timothy Marko.
Rais wa jamuhuri ya muungano Wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteua Seperatus Fella kuwa katibu mkuu wa sektetariteti ya kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu .
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam Msemaji wawizara yamambo ya ndani ISAAC Ntanga amesema kuwa uteuzi wa Seperetus Fella unafuatia kuuundwa kwa kamati yakuzuia biashara haramu ya mwaka 2008 ikiwa nalengo lakudhibiti biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu .
‘’Chimbuko la kutungwa kwasheria yakuzuia Biashara haramu ya usafirishaji binadamu ni itifaki ya kimataifa yakuzuia kupambana na kutoa adhabu kwa watekelezaji wa biashara ya usafirishaji haramu ya binadamu hasa wanawake nawatoto’’Alisema Isaac Ntanga .
Ntanga alisema kuwa itifaki hiyo ni nyongeza ya mkataba wa umoja wamataifa dhidi yauhalifu wa kimataifa wa kupangwa ambapo serikali ya Tanzania imeridhia mkataba huo ikiwemo na itifaki yake.
Alisema kuwa juhudihizo za serikali ya Tanzania zinaendana na tamko lakimataifa la haki za binadamu na lile la mkataba wa kimataifa wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na mkataba wa haki za watoto wa mwaka 1989.
‘’Makosa yanayo vunja sheria yakuzuia usafirishaji haramu wa binadamu nipamoja nakupanga ,kupangisha nyumba au kutumia jengo kwa ajili yabishara yabinadamu nakugushi hati kwa madhumuni kukuza biashara haramu ya binadamu .’’Aliongeza Ntanga .
Aliongeza kuwa adhabu ya wanao tiwa hatiani kwakunja sheria hiyo nipamojana kifungo cha mwakamoja au kisishozidi miaka saba au fani isiyo zidi milioni mbili au milioni hamsini au vyote kwa pamoja .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni