Timothy Marko
KUFUATIA kuwepo kwa madai ya kupekuliwa kwa wageni wa kutoka katika nchi za bara za asia ikiwemo warabu wahindi katika wanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere jijini hapa na baadhi ya wafanyakazi wanaolinda wanja huo Serikali imewafukuza watumishi 14 wanafanya kazi katika wanja huo kwa kukutwa nakuhusika navitendo vya rushwa .
Akizungumza jijini leo na waandshi wa habari Waziri wauchukuzi nchini Harrison Mwakyembe amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa MWALIMU JULIUS NYERERE kukagua na kuwa bagua wageni wanaotoka nchini china ,wahindi na warabu kwa minadi yakuwa bidhaa zao haziruhusiwi kuingia hapa nchini ambapo baadhi ya wafanyakazi hao huwatoza fedha kutokana ilikuweza kuruhusu bidhaa hizo.
‘’Hivi karibuni kumekuwa naubaguzi wa wageni wa kutoka china ,pamoja wahindi nawaarabu kuwa wanakaguliwa bidhaa zao ambapo baadhi yawafanyakazi wanaolinda wanja wandege huwatoza fedha ilkuweza kusafirisha bidhaa zao ‘’Alisema Mwakyembe .
Mwakyembe alisema kuwa Baadhi ya maafisa hao katika Uwanja huo hudaiwa kuwa kutoa huduma yachanjo ya ugonjwa wa homa ya manjano nakusababisha msongamano katika wanja huo wakimataifa wandege hasa kipindi cha mchana nakusababisha msongamano wandege zinazotua katika uwanja huo .
Alisema kufuatia tukio hilo amewaagiza watumishi mbalimbali wakiwemo wauguzi kuvaa sare maalumu ambazo zinazo akisi (Refletor).
Katika hatua nyingine Waziri huyo amewaondoa watumishi 11 Wakiwemo watumishi sita wanaotoka wizara yakilimo na watumishi tano kutoka wizara ya afya na watumishi wawili kutoka wizara ya mifugo nauvuvi .
‘’Watumishi wa wizara ya kilimo waliondololewa ni pamoja na Teddy I.Mwasenga ,Esther Kilonzo ,Rehema Mrutu,Mary Kadokayosi, Kisamo S.samji na Anneth Kiliyanga Watumishi wa wizara ya afya ni pamoja na Agness Shirima ,Hamis Bora,Valeri C.Chuwa ,Elingaera na Remedius Kakulu Wakati watumishi wawizara mifugo nauvuvi ni Elishi Samson NDOSI, Anne I.Setebe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni