Ijumaa, 27 Juni 2014

UTENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA NCHINI WATILIWA SHAKA

Timothy Marko.
IMEELEZWA  kuwa hali yautendaji katika serikali za mitaa nchini imekuwa si yakuridhisha nakuweza kusababisha kuwepo utendaji hafifu wa watendaji mbalimbali wa taasisi mbalimbali za serikali za mitaa hapa nchini .
Akizungumza jijini leo katika kongamano lililo andaliwa na taasisi inayoshugulika nakuratibu  sera Policy Forum Mbunge wa jimbo la Ole mjini  Zanzibar na mwenyekiti wa kamati yahesabu za serikali za mitaa, Rajabu Mbaruku amesema kuwa hali yauwajibikaji imefikia asilimia hamsini ambapo lengo nikufikia asilimia miamoja .
‘’Hali yanchi za afrika katika dhana yauwajibikaji tumefikia asilimia hamsini ambapo lengo nikufikia asilimia mia moja katika utendaji na uwajibikaji hali hii si yakuridhisha hata kidogo hii inatokana nanchi za afrika nyingi  kujenga mazingira ya kulindana’’Alisema Rajabu Mbaruku.
Mbaruku alisema kuwa wananchi kama wananchi wanapaswa kutambu ahaki zao ambapo hivi karibuni tumekuwa tukilipigia kelele mawaziri mizigo lakini bado swalahili halijapatiwa ufumbuzi .
Alisema kuwa kumekuwa na matatizo katika kupata habari kutoka kwa Mkaguzi mkuu wa mahesabu yaserikali (CAG)kuhusiana taarifa za mapato na matumizi katika serikali za mitaa taarifa za CAG haziko wazi kama hivi karibuni tulihoji juu mapato namatumizi ya shilingi bilioni 15 .
‘’Hadi hivisasa hatujaweza kupata taarifa yafedha juu ya matumizi ya shilingi biloni 15 sisi kama wabunge waupinzani tutaleta mswada wa vyombo vyahabari ilivyombo vyahabari vipewe uhuru wakuhoji maswala kama haya’’Aliongeza Rajabu Mbaruku .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa hesabu zaserikali za mitaa Rajabu
Mbaruku alishangazwa namswada wavyombo vya habari kupigwa kalenda kujadiliwa bungeni wakati Rais jakaya kikwete Alisha ahidi kuwa mswada huo utaletwa bungeni ilkuweza kujadiliwa lakini jambo hilo halijatekelezwa hadi hivi sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni