Jumatano, 11 Juni 2014

JESHI LAPOLISI NCHINI LAWASHIKILIA WATU SITA KWA KUMUUWA ASKARI POLISI

Timothy Marko
Katika kuhakikisha  usalama wa raia na mali zao vinatekelezwa  ,Jeshi  la  polisi nchini limeanzisha msako mkali wa watu wanaodhaniwa ni majambazi katika wilaya ya mkuranga mkoani pwani baada ya majambazi hao kumjerui na aliyekuwa askari polisi wilaya hiyo koplo Joseph Ngonyanimweye namba za usajili D.9887 na baadaye kufariki katika hospitali ya wilaya ya mkuranga ambapo askari huyo alipokuwa akipatiwa  matibabu.
Akizungumza mapema leo jijini, Kamishina wapolisi nchini Paul Chagonja amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana usiku majira ya saa saba usiku katika kijiji cha Kimanzichana mkoani pwani   ambapo  zaidi ya watu sita wanaodhaniwa ni majambazi wa livamia kituo cha makamba kilicho po mkoani humo na kupora silaha aina ya shotgun 3za kiraia na SMG 2 za jeshi la polisi zikiwa na risasi 30.
‘’ Jeshi lapolisi linawashikilia watu sita mkoani Pwani  wanaodhani wa kuwa ni majambazi waliovamia kituo kidogo cha polisi cha Mkamba nakupora silaha aina ya shot gun 3 za kiraia na SMG2 za kijeshi zikiwa narisasi 30ambazo zilikuwa kwenye ghala lamuda zikisubiriwa kupelekwa kwenye kituo kwenye ghala kuu la silaha’’Alisema Kamishna Paul chagonja.
Kamishina Chagonja alisema majambazi hao walijerui askari wawili ambao walikuwemo katika kituo hicho ambao venance Franicis na Mariam Makamba ambao bado wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
Alisema kuwa jeshi lapolisi linalani kitendo hicho nakuamua  kufanya msako mkali na kuwasaka watuhumiwa hao nakuwa tia mbaroni majambazi hao ili kusudi hatua zakisheria zifuatwe ikiwemo kuwapeleka mahakamani.
‘’Natoa wito kwa wananchi kuwa watulivu nakuendelea kutoa ushirikiano kwa polisi wakati uchunguzi unaendelea ,nawaomba raia wema wapige namba 0754 785557 au 0715009953 kwa kamanda wa mkoa wapwani Ulrich Matei pindi watakaposikia taarifa za wahalifu hao ‘’Alisema kamishina Chagonja .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni