Jumanne, 24 Juni 2014

JESHI LAPOLISI KANDA MAALUM YATANGAZA MSAKO MKALI KUFUATIA MAUAJI YA MTAWA

Timothy Marko.
KUFUATIA  kuwawa  nakupigwa risasi kwa aliyekuwa mtawa wa kanisa katoliki Sista Cresenscia Kapuri (50)juni 23 mwaka huu huko Ubungo kibangu jeshi lapolisi kandamaalu jijini Dar es salaam limetangaza msako mkali na kuwatafuta watuhumiwa walio husika na mauaji ya mtawa huyo.
Akizungumza jijini leo kamishina wapolisi kanda maalum ya Dar es salaam Suileiman Kova amesema kuwa awali marehemuhuyo alikuwa ameongozana na wenzake ambao ni sista Brigita Mbaga(32)mkaazi wa makoka wakiwa nadereva wao Mark Partick Mwarabu akiwa akiendesh
a gari ainaya Pick-up/T Hilux yenye namba T213 wakitokea katika benki ya CRDB tawi la mlimani city ambapo walipofika katika eneo laubungo kibangu ilikulipia deni lachakula katika duka la Thomas Francisis ndipo walitokea majambazi wawili wakiwa napikipiki ambayo hakuweza kusomeka namba ndipo jambazi mmoja mwenye bunduki aina ya SMG walipiga risasi kidolegumba cha mkono wa kulia wadereva wagari hiyo nakisha kupiga risasi mtawahuyo kifuani nakuwaweza kufanikiwa kupora kiasi cha shilingi milioniishirini .
KamandaSuleiman kova amesema kufuatia tukio hilo jeshi lake limegundua kuwa matukio yaujambazi yanayohusiana majambazi kuporwa kiasi kikukubwa cha fedha huanzia kwenye mabenki ambapo majambazi hao huwafuatilia wateja wanaoingia nakutoka katika mabenki mbalimbali .
‘’Imeonekana kwamba maranyingi mabenki yanahitaji kusafirisha pesa nyingi hutumia escort yapolisi ama taasisi nyinginezo zinazotoa huduma hiyo ya ulinzi .’’Alisema Suleiman Kova.
Kamanda kova alisema nimuhimu kwa wateja wamabenki kutochukua kiasi kikukubwa cha fedha hali hiyo inaweza kusababisha kuporwa kwa fedha kirahisi na watu wasio waaminifu .
‘’Mabenki ya wahawahimize wateja wake kutumia hundi katika kufanya mihala bila kadi pamoja nanjia nyinginezo za kifedha ‘’Aliongeza kova
Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kupatikana namadumu yapatayo 28 yakiwa namafuta yadizeli yenye ujazo lita 40 ambayo mali hiyo imepatikana kwanjia ya wizi aidha kamanda kova amesema tukio hilo lilitokea June20 Mwaka huu katika maeneo yavijibweni katika matanki yakuhifandhia mafuta wilaya kipolisi kigamboni mkoa wa TEMEKE.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni