Na Timothy
Marko.
Maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani yanatarajiwa kufanyika kesho ambapo mazimisho hayo
hufanyika kila mwaka march 8 ambapo katika madhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa
kufanyika katika viwanja vya Mwembeyanga manispaa ya Temeke.
Akizungumza
nawaandishi wahabari jijini leo, mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es salaam Said
meck Sadiki amesema maadhimisho hayo yanaendana nakaulimbiu ijulikanayo kama
chochea mabadiliko kuleta usawa wakijinsia aliongeza kuwa ujumbe huo unalengo
la kuhamasisha wanaume na wanawake pamoja na asasi za kiraia pamoja nazile kidini
kuhusiana ushirikishwaji katika ngazi za maamuzi.
‘’ujumbe huu
unaelimisha nakuhamasisha jamii ,serikali ,asasi zakiraia pamoja na asasi za
kidini kuhusu umuhimu wa kushirikiana wanaume na wanawake katika ngazi ya
kijamii ,kisiasa nakiuchumi katika kutoa fursa sawa katika mkoa huu nataifa
kwajumla’’alisema said Meck sadiki.
Mecksadick
alisema kuwa lengo laujumbe huo nikuwakumbusha kwajili ya kupambana
nachangamoto mbali mbali wanazo kumbana wanawake ambapo alizitaja moja ya
changamoto hizo nikutopewa haki sawa katika ngazi za maamuzi aukutoshirikishwa
kikamilifu.
Aliongeza
kuwa wanawake wamekuwa namchango mkubwa wakulea familia lakini wanaathirika
zaidi namaradhi mbalimbali yakiwemo ukimwi ,vifo vitokanavyo nauzazi ,kupigwa
,kutukanwa nakubakwa, ukeketaji, mauaji yavikongwe, mimba za utotoni,pamoja
nakunyimwa haki ya kumiliki mali.
‘’mnamo
febuary6 mwaka huu ulifanyika uzinduzi katika uwanja mwembe yanga ambapo
vikundi mbalimbali vyaujasiliamali bado vina endelea kuonesha bidhaa zao za
ujasiliamali katika uwanja huo ambapo wadaumbali walikuwepo’’.aliongeza mkuu
wamkoa .
Aliwataja wadaumbalimbali walishiriki kuwani benki
yaposta ,benki yawananchi ambapo wanaendelea kutoa elimu mbalimbali ikiwermo
utunzaji fedha namikopo nakuongeza kuwa wadau wengine ni tume ya kudhibiti
ukimwi nataasisi inayojishulisha namsada wakisheria ya Equal for Growth.
Samba mba
nahilo mkuu wa mkoa alisema, kutakuwa na maandamano ambapo maandamano hayo
yataanza kwenye magorofa ya Tandika hadi viwanja vyamwembe yanga nakupokelewa
ambapo mgenirasimi anatarajiwa waziri utumishi wa umma hawa ghasia.
‘’kama
ilivyo ada ya desturi yetu wananchi wote mkoa wa Dar es salaam mnaombwa
kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maadhimisho haya kwa kuzidi kutafakari kauli
mbiu ya mwaka huu isemayo chochea mabadiliko kuleta usawa wakijinsia’’.alisema
Mecksadiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni