Alhamisi, 4 Agosti 2016

SERIKALI KUWA CHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATAKAO KIUKA SHERIA ZA BARABARANI.



Timothy Marko .
KATIKA kuhakikisha ajali za barabarani zinatokomezwa nchini ,Serikali imesema kuwa haitosita kuwachukulia hatua madereva watakao kiuka sheria za barabarani ikiwemo kuwapeleka mahakamani na kuwafungulia mashitaka .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema kuwa madereva wanaoendesha boda boda watakao kiuka sheria za barabarani ikiwemo kupandisha abiria zaidi ya wawili maarufu mshikaki jeshi la polisi litachukua hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo nakuweza kumpeleka Mahabusu.

‘’kumekuwa natabia ya madereva wa boda boda wamekuwa na tabia ya kubeba mshikaki tumeweka sheria kali ikiwemo kuwafungulia mashitaka nakuwapeleka mahabusu nakisha mahakamani ‘’Alisema Naibu Waziri Masauni Masauni .

Masauni alisema kuwa sambamba nakutoa adhabu kwa madereva wa boda boda pia jeshi la polisi halitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa mabasi ya abiria ambao abiria wake hawafungi mkanda .

Alisema Katika suala hilo jeshi la polisi halitomchukulia hatua za kisheria dereva pekeyake bali hata abiria ambaye atakaye onekana hajafunga mkanda .

‘’Sambamba na sheria hizi ,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani tutaendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ikiwemo kuonesha maeneo yote tete yanayosababisha ajali kwa kushirikiana na Tan roads’’Aliongeza Masauni .

Aliongeza kuwa jeshi la polisi litaendelea kuwa chukulia hatua wale wote waliokuwa natabia yakuweka vioo vilivyotiwa giza (tinted)ilikuweza kupunguza tatizo hilo la ajali .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni