Timothy Marko.
JESHI lapolisi Kikosi cha usalama Barabarani nchini imewataka Madereva wa Boda boda kuizingatia Sheria na usalama wa abiria pindi wanapo fanya shughuli zao zakujitafutia kipato .
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina Msaidizi wa Kikosi chausalama barabarani Fotunatus Musilm amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha hali inayochangiwa na madereva hao kutozingatia sheria za barabarani pindi wawapo katika shughulizao za kujitafutia kipato.
''Kutoa elimu kwamadereva wa bodaboda na Bajaji nimuhimu katika kupunguza vifo vyawatanzania watanzania wengi wamekuwa wakipoteza maisha hali inayochangiwa na madereva waboda boda kutozingatia sheria za barabarani ''Alisema Kamishina Fotunatus Musilim
Kamishina Musilim alisema kuwa nivyema madereva wabodaboda kuzingatia sheria za usalama barabani ilikuepukana navifo naajali nakuwataka madereva boda boda kuendesha kwakuzingatia hali yakusalama pindi wawapo barabani .
Alisema sambamba nakutoelimu kwa madereva hao kuzingatia sheria jeshi hilo limewataka kuanzisha benki nasacoss mbalimbali zitakazowawezesha kiuchumi na kuondokana na umasikini.
''hivi karibuni tunatajia kuandaa mashinano ya Mipinga Cup lengo nikuwahamasisha waendesha bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani ''Aliongeza Kamishina Msaidizi Musilimu .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni