Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, Jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu |
Wizara ya
Afya Maendeo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto imepiga marufuku matumizi ya
vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayojiuhusisha mapenzi ya
jinsia moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam jana Waziri wa Afya Maendeleo ya
jamii, Jinsia,wazee na watoto Ummy
Mwalimu alisema vitendo vya mapenzi ya
jinsia moja ni kinyume na sheria zilizoweka nchini na pia avitambuliki kabisa.
Alisema serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo
ambavyo vimekuwa vikitumiwa na baadhi ya
makundi yanayojiusisha na mapenzi ya
jinsia moja ili kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU.
“Kipaumbele
cha serikali hii ni kujenga wodi za akinamama,kununulia vifaa vya kujifungulia
pamoja na ununua madawa hospitalini
na sio kutoa fedha kwa ajili ya
vilainishi kwa makundi hayo”alisema.
Ummy alisema
kuwa vitendo hivyo ni kinyume na maadili ya kitanzania pia serikali haitambui
vitendo hivyo ambavyo vimekuwa ni kinyume na dini zote nchini.
Alisema
makundi hayo yapo hatarini kwa kiasi kikubwa kupata maambukizi mapya ya VVU
kutokana na kujijusisha na vitendo hivyo
kwa kasi zaidi.
Ummy alisema
kuwa takwimu zilizopo zinaonbesha kuwa mkoa wa Dar es salaam pamoja na Dodoma imekuwa
ikiongoza vitendo hivyo yvya mapenzi ya jinsia moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni