Alhamisi, 13 Oktoba 2016

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA CHINA KATIKA KUPITIA MAGEUZI YA KIUCHUMI





Timothy   Marko
WAKATI  Serikali ya awamu yatano ikiweka msisitizo mkubwa  juu yakujenga uchumi kupita sekta ya viwanda nchini, Tanzania pamoja na serikali ya china leo wameingia makubaliano ya shilingi bilioni 97 ilikuweza kuinua sekta hiyo katika mikoa yapwani.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda wakutoka nchini china pamoja na Tanzania jijini  Dar es salaam Waziri wa viwanda na Biashara Charles Mwijage amesema kuwa fedha hizo zitajumuisha katika kufanya maboresho ya ujenzi wabandari ya bagamoyo na kuweza kuboresha miundombinu  ya reli ya kati sambamba naujenzi wa bandari ya Zanzibar.


PICHA: Waziri Mwijage kulia pamoja na naibu waziri wa biashara wa china Qian Kieming.

‘’Hali ya ukuaji wa uchumi inaendana sambamba naukuwaji wasekta ya viwanda ili kuiwezesha nchi ya Tanzania kufikia malengo yake ya nchi ya uchumi wakati sekta ya viwanda hainabudi kuwekewa mkazo ,serikali  kwa kulitambua hilo mwaka huu na mwaka ujao imelenga kuleta mageuzi ya uchumi kupitia sekta ya viwanda ‘’Alisema waziri wa  viwanda nabishara Charles Mwijage.

Waziri Mwijage alisema kuwa katika kuhakikisha Tanzania inafikia katika uchumi wa viwanda imelenga kutumia fedha hizo katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kiwandachavigae katika wilaya mkuranga ambapo jumla ya dola milioni 150 zinatarajiwa kujenga kiwanda hicho.
Alisema sambamba naujenzi wa kiwanda cha vigae katika mkoa wa pwani piaserikali kwakushirikiana na nchi ya china inatarajiakujenga viwanda vya nguo chenye urefu wakilometa za mraba 2,400.

‘’tutandelea kukuza uhusiano wetu kati yetu na nchi ya china kwani uhusiano wetu na china niwakitambo kirefu tangu enzi za uhuru 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni