Mr. Khalfa Rehan meneja wa Bina ya Afya wa Jubilee insurance habari wa hospitali . |
Timothy Marko.
KATIKA kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya tiba ya moyo nchini ,Hospitali ya Agakhan imesema kuwa inaendelea kutoa huduma ya matibabu ya ugonjwa wamoyo nchini pasipo kuwapeleka wagonjwa wa ugonjwa huo katika nchi za Asia kama ilivyokuwa awali .
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Meneja Mkuu wa kitengo cha huduma za dharura katika hospitali hiyo Lucy Adhiambo amesema kuwa hospitali hiyo tayari imanza kufanya matibabu yaupasuaji wa moyo unaoendana sambamba nakufungua mishipa iliyopo katika moyo .
''Kwakutumia mashine za kisasa kabisa hospitali yetu inafanya uchunguzi wa matibabu yamoyo kwa kuangalia moyo unafanyaje kazi ambapo katika kipindi cha mwezi october tayari taasisi yetu imewahudumia wagonjwa 300 ambapo kwa wastani kila mwezi ni wagonjwa thelathini ''Alisema Mkuu wa Kitengo cha dharura Lucy Adhiambo .
Kutoka kulia nia Afisa masoko na mawasiliano wa hospital ya Aga khan jijini Dar akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mapema leo, kushoto ni Mr. Khalfa Rehan meneja wa Bina ya Afya wa Jubilee insurance habari wa hospitali . |
Mkuu wa kitengo cha Dhalula Adhiambo alisema kuwa taasisi hiyo hutoa huduma za upasuaji wamoyo kwa watu wote ikiwemo watoto wadogo walio kati ya umri wamiaka mitano nakuendelea .
Alisema Endapo Mgonjwa anahitaji huduma kubwa zaidi yaupasuaji wa moyo taasisi hiyo humpeleka katika hospitali ya rufaa yamuhimbili ilkuweza kupata uchunguzi zaidi juu ya ugonjwa huo .
''huduma za watoto za moyo zipo lakini zimekuwa zikipatikana na endapo mtoto anakuwa nashida kubwa ya upasuaji wa moyo huwa tunampeleka katika hospitali ya rufaa ya muhimbili ''Aliongeza Lucy Adhiambo.
Aidha ,katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Jubblie Insurance Alpha lekhan amewataka wananchi nchini kujiunga na bima yaafya kutoka katika taasisi hiyo ilikuweza kutibiwa magonjwa makubwa ambayo yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha ikiwemo Saratani .
Lekhan Alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitoa bima ya afya kwa kumlipia mgonjwa yeyote hadi kiwango cha matibau ya magonjwa mbalimbali yenye gharama kwa kiasi cha shilingi milioni 150 kwamwaka .
''Gharama hizi zinajumuhisha matibabu ya Ward ,Matibabu ya HIV, Ajali Matibabu ya gharama za maabara ,huduma za uzazi ikiwemo Matenity kwa mwanachama aliyejiunga na mfuko wetu tunatoa '' Alisema Mkurugenzi lekhan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni