Alhamisi, 15 Septemba 2016

WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA TAMASHA LA WAJASILIAMALI 0CTOBER 31 .

Tokeo la picha la ujasiliamali
BAADHI YA WANAWAKE WAKIFANYA SHUGHULI ZA UJASILIAMALI
Timothy Marko.
WANAWAKE nchini wametakiwa kujitokeza katika matamasha mbalimbali yahusuyo ujasilimali ilikuweza kukuza uchumi nakuwajengea uwezo wa kuyafikia masoko mbalimbali nje na ndani yanchi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tamasha la Wanawake wajasiliamali nchini (MOWE)Elihaka Mrema wakati akitoa taarifa yake kwa vyombo vyahabari juu ya Maandalizi ya Tamasha la wanawake wajasilimali nchini linalotarajiwa kuanza  October 31 hadi November 5mwaka huu katika viwanja vyamnazimoja jijini Dar es salaam.

''Tamasha hili linalenga kuwasaidia wanawake wajasilimali kukutana nawatoa huduma za uendeshaji wa biashara ikiwemo TRA ,BRELA,TFDA ,VIPIMO ,GSI naTBS ilikuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanawake kiuchumi''Alisema Mwenyekiti Elihaka Mrema.

Mwenyekiti Elihaka alisema kuwa kutokana namchango mkubwa wa shirika la kazi duniani taasisi hiyo imekuwa namafanikio makubwa ikiwemo kuwepo kwa wanawake wengi walihamasika katika shughuli za ujasiliamali .

Alisema kutokana natamasha hilo la MOWE kumekuwa naukuwaji wa masoko ya bidhaa na huduma za wajasiimali wanawake ikiwemo upatikanaji wamasoko katika ukanda wa afrika mashariki ,afrika  Marekani ,asia Pamoja naulaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni