Ijumaa, 23 Septemba 2016

PPF KUENDELA KUFANYA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHINI .

AFISA UHUSIANO  WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF LULU MENGELE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI   JUU YA  ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHINI .


Timothy Marko.
MFUKO wa Pensheni nchini (PPF)unatarajia kuendelea  na uhakiki  wa wastaafu kuanzia Jumatatu ijayo katika  mikoa ya kanda Mashariki na kati, Morogoro ,Dodoma na Singida .

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Meneja Kiongozi wa Pensheni na Huduma, John Mwalisu,amesema kuwa uhakiki huo unaendelea mikoa mingine baada ya kumalizika Dar es Salaam.

‘’Uhakiki wamikoa mingine ya wastaafu nipamoja na Kanda ya ziwa katika mikoa ya Mwanza ,Mara ,Kagera ,kigoma mjini ,shinyanga mjini ,Tabora mjini Geita mjini  ,Simiyumjini ,Maswa pamoja na mkoa wa bariadi ‘’Alisema Meneja kiongozi Jonh Mwalisu .

Meneja Kiongozi Mwalisu alisema kuwa mikoa mingine itakayo husika katika zoezi hilo ni Kuanzia october 17 hadi 21 nipamoja na Mikoa ya nyanda za juu kusini ambapo aliitaja mikoa hiyo nipamoja na Mbeya,Iringa pamoja na Rukwa .

Alisema kuwa zoezi jingine la uhakiki wastaafu linatarajiwa kufanyika Oktober 24 hadi 28 katika mikoa ya Arusha,kilimanjaro ,Manyara wakati kanda ya kusini inajumuisha mikoa ya Mtwara mjini ,Newala ,Masasi ,lindi mjini ,Ruvuma Mjini pamoja na tunduru inatarajiwa kufanyika kuanzia OKutoba 24 nakuishia okutoba 28.

‘’Zoezi hili linawataka wastaafu wote kuja nanyaraka zifuatazo Kitambulisho cha mstaafu cha PPF ,Picha moja ndogo ya rangi ya sasa ,kitambulisho chataifa ,kadi yampiga kura ama hati ya kusafiria  au leseni yaudereva ‘’Aliongeza Mwasu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni