Timothy
Marko.
KATIKA
kuhakikisha Agizo la Rais wa awamu tano wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kuyaweka mazingira katika hali ya usafi
wafanyakazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA)wamefanya usafi katika
nyumba zinazo kaliwa na wafanyakazi hao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa
taasisi hiyo, Elius Mwakalinga amesema kuwa hatua yawafanyakazi hao kufanya
usafi katika maeneo yanayozunguka nyumba zinazokaliwa na wafanyakazi hao
kunafuatia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika mashirika na taasisi
zinazomilikiwa na serikali .
‘’Sisi kama
Wakala wa Majengo ya serikali tumeamua
kutekeleza agizo la Mheshimiwa Dkt.Magufuli la kudumisha usafi katika maeneo
yetu ambapo hii leo tupo hapa Mikocheni Mtaa wa Alhaj Muhaj ambapo nyumba hizi
zimekuwa zikimilikiwa na Mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali,” alisema
Mwakalinga.
Katika hatua
nyingine Mwakalinga alisema taasisi hiyo inaendelea kuwafuatilia wateja wake
ambao hawajalipa kodi za majengo ambapo katika Mkoa wa Mwanza jumla ya wadaiwa
sugu wa majengo 27 wanadaiwa na TBA.
Alisema kuwa
taasisi hiyo inawadai wateja wake takribani shilingi bilioni 16 katika vipindi tofauti.Hata hivyo hatuja pata takwimu sahihi kwa wadaiwa sugu waliopo jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Kitengo cha Habari TBA , Edina Joseph amesema kuwa zoezi hilo lakuwafuatilia
wadau sugu linaendelea katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani .
Alisema kuwa
hatua ya taasisi hiyo kufanya usafi katika maeneo ya nayozunguka katika nyumba
zinazomilikiwa nataasisi hiyo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni