Jumatano, 25 Mei 2016

SHILINGI MILIONI750 ZAKUSANYWA MAY JIJINI ARUSHA .


Timothy Marko.

JUMLA shilingi milioni 750 zimekusanywa kipindi cha mwezi moja katika Halimashauri ya jiji la  Arusha ambapo makusanyo yafedha hizo zimetokana na tozo mbalimbali kama kodi kwanjia yamfumo wa kieletroniki unaotumiwa na benki yakibiashara National Microfinance Bank (NMB).

 

Akizungumza nawaandishi wahabari kwanjia yamtandao jijini Arusha Mkurugenzi wa halimashauri yaarusha Juma Idd amesema kuwa makusanyo yafedha hizo yametokana nakodi za majengo leseni pamoja na maduka mbalimbali yalipo katika jiji hilo .

 

‘’Makusanyo haya ya shilingi milioni 750 yametokana najuhudi mbalimbali za halimashauri  yajiji la ARUSHA kwakuweza kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji hili la arusha kwa kutumia njia yamfumo wa kieletroniki ambapo mfumo huu umewezesha kukusanya taarifa nyingi za walipa kodi katika halimashauri yajiji hili ‘’Alisema Mkurugenzi Juma IDD .

 

MKurugenzi IDD amesema kuwa mfumo huo umeweza kuepusha njia za panya za ukwepaji kodi kwa watumishi wa mamlaka ya ukusanyaji kodi kutoza kiwango ambacho hakiendanisawa na mapato ya wafanyabishara hao nakuondokana na kadhia ya wafanyabishara hao kubeba fedha nyingi kuweza kulipa kodi .

 

Alisema kuwa mfumo huo umeweza kumrahisiashia mlipa kodi nchini kuweza kutumia hundi ilikuweza kulipa kodi katika manispaa hiyo ya Arusha ,kwakushirikina nabenki ya NMB Kumewezesha kurahisha ukusanyaji wa mapato katika halimashauri hiyo.

 

‘’Mwananchi anaweza kulipa kodi popote kwakutumia mifumo ya kieletroniki  ile risiti yamalipo inatolewa kwasekunde tisini ambapo awali ilikuwa kwamuda saa moja hadi matatu njia hii ya ulipaji kodi inafanyika kwanjia ya NMB Mobile pamoja na kushirikiana namitandao yasimu nchini ‘’Aliongeza  MKURUGENZI JUMA IDD.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni