Timothy
Marko.
JESHI la
polisi nchini limetoa miezi mitatu kwa wananchi wanaomiliki silaha kuhakiki
silaha zao nakulipa ada ya umliki wa silaha hizo .
Akizungumza
na Waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina wa operesheni
na mafunzo CP Nsato Mssanzya amesema kuwa Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo
kwa mkanganyiko wa operesheni yaukaguzi wasilaha hizo kwa mikoa mbalimbali
nchini.
‘’ZOEZI
laukaguzi wasilaha limekuwa rikiratibiwa
nakila mkoa kwakutoa muda wake kibinafsi jambo ambalo limeleta mkanganyiko katika
utekelezaji wa zoezi hilo kwa baadhi ya wamiliki ‘’Alisema Kamishina
waoperesheni na mafunzo CP Nsato Mssanzya .
Alisema kuwa
sambamba nazoezi hilo pia jeshi hilo limewatahadharisha wananchi kuwa makini
navitendo vya kihalifu katika maeneo yao ikiwemo kubaini makundi mbalimbali ya
kihalifu katika maeneo yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni