Ijumaa, 4 Machi 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AYATAKA MAKAMPUNI YA WAFANYABISHARA KUTANGAZA BIASHARA ZAO KUPITIA WA UWANJA WA TAIFA.



Na Lilian Lundo - Maelezo

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameyataka makampuni na wafanyabiashara kutangaza biashara zao kupitia uwanja wa Taifa.
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo jana katika mkutano wa wadau wa michezo wakiwemo wadhamini wa michezo, vyama vya michezo vya Taifa na mashirikisho  uliofanyika katika moja ya kumbi zilizopo uwanja wa Taifa.
“Uwanja wetu una hadhi ya kimataifa lakini uwanja huu hautumiki kutangaza biashara yoyote  kama chanzo cha mapato, badala yake kuta za  uwanja  zimezungukwa na giza hasa muda cha usiku,” alisema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa aliongeza kwa kusema kuwa  kama uwanja huo utazungukwa na mabango ya matangazo yataupandisha  hadhi  na kubadilisha mandhari ya uwanja hasa muda wa usiku na  fedha zitakazopatikana zitatumika kuboresha uwanja huo.
Hivyo Mhe. Majaliwa amewataka wadhamini wa michezo kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ya kutangaza bidhaa au huduma wanazozitoa kupitia uwanja wa Taifa ambao hutumika katika mechi nyingi za kitaifa na kimataifa zinazochezwa nchini.
Aidha, Mhe. Majaliwa amesema kuwa Tanzania itaendelea kupata heshima kupitia sekta ya michezo kwani michezo ni kielelezo kinachoweza kutambulisha utamaduni wa Taifa hivyo wadau wa michezo washikamane na Serikali na kuona ni namna gani matatizo ya michezo yatatatuliwa na michezo kuendelezwa nchini.
Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuendeleza michezo nchini kwa kuweka misingi imara ya kuendeleza michezo kuanzia umri wa chini, kurekebisha sera na sheria za michezo ziliopitwa na wakati, kujali mafanikio, matatizo na mambo muhimu yanayohusu michezo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni