Timothy Marko.
KATIKA
kuhakikisha afya za wananchi wa mkoa wa Dar es salaam zinaimarika nakuondokana
natatizo la kipindu pindu ,Afisa afya mkoa huo amewataka watendaji wa ngazi ya
wilaya zote kuweza kuboresha hali ya vitendea kazi ilkuweza kuboresha hali ya
usafi .
Akizungumza
katika mkutano wa watendaji wa manispaazote , mkoa Dar es salaam Afisa afya
Bakari Mhina amesema kuwa nivyema
serikali ikaunda idara ya mazingira itakayo simamia masuala ya usafi katika
kata zote katika mkoa huo .
‘’Tunaiomba
serikali iweze kuandaa idara yausafi na mazingira ambayo itaainisha majukumu ya
idara hii kwani hali yausafi sio ya kuridhisha katika mkoa wetu ‘’Alisema Afisa
afya BAKARI MHINA.
Afisa afya
MHINA alisema kuwa uundwaji wa idara hiyo kutwezesha kuimarisha hali yausafi
katika kata zote za mkoa wa Dar es salaam .
Alisema kuwa
pamoja na kuzitaka manispaa hizo kudumisha hali ya usafi katika mkoa wa Dar es
salam pia ameongeza kuwa atazitafutia ufumbuzi wa changamoto za vitendea kazi
ikiwemo rasmali fedha katika kudumisha usafi .
‘’Nafahamu
changamoto mlizonazo katika kutekeleza suala hili linahitaji vifaa na rasmali
fedha nitawasilisha mapendekezo yenu katika serikali kuu ilikuweza kutatua
changamoto hizi ‘’Aliongeza MHINA.
Afisa afya wilaya ya Temeke Irene Chuwa alizitaja changamoto
zilizopo katika wilayayake kuwa wilaya hiyo inakabiliwa natatizo lauchafu hali
inayotokana nakuwepo kwa wakandarasi wachache wakufanya shughuli hiyo .
Alisema kuwa
sambamba nauhaba wa wakandarasi pia wiaya hiyo inakabiliwa na uhaba wa vitendea
kazi ili kufanikisha suala zima la usafi .
‘’Katika
wilaya yetu ndugu mwenyekiti tunakbiliwa na changamoto ya uhaba wa wakandarasi
wa kuzoa taka na uhaba wa vifaa vyakufanyia usafi ‘’Alisema IRENE CHUWA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni