Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 7 Desemba 2015
WATUMISHI WATAKIWA KUTEKELEZA AHADI ZAO ZAVIAPO KWA VITENDO.
Timothy Marko .
WATUMISHI wa umma nchini ,wametakiwa kutekeleza kwa vitendo ahadi za viapo vya uadilifu pindi wawapo katika sehemu zao za kazi ilikuweza kuleta maendeleo yenye tija kwa Taifa .
Kauli hiyo imetolewa hii leo jijini Dar es salaam na katibu mkuu wa utumishi wa umma HAB Mkwizu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya Habari MAELEZO ambapo aliwataka watumishi wa umma kusoma na kuzingatia waraka uliotolewa na ofisi yake kuhusiana na suala zima la uadilifu .
‘’Kila Mwajiri katika utumishi wa umma anapaswa kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyomo katika waraka wa mkuu wa utumishi kuhusu ahadi za uadilifu ‘’Alisema Katibu Mkuu HAB MKWIZU .
Katibu Mkuu MKWIZU alisema kuwa viapo hivyo vina walenga watumishi ikiwemo waajiri wote katika kufanya utekelezwaji wa magizo yaliyo tolewa na ofisi hiyo.
Alisema katika kuzingatia madili hayo, kila mtumishi anatakiwa kusaini kiapo kinachohusiana nawatumishi kuzingatia sheria na taratibu za mazingira yaeneo husika .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni