Jumanne, 8 Desemba 2015

UKATILI WAKIJINSIA WAWA KAA LAMOTO KWA TANZANIA .

Timothy Marko. KATIKA kuelekea kilele cha Maadhimisho yasiku ya haki za binadamu nchini Tume ya Haki za binadamu nchini Desemba 10 mwaka huu Tanzania imeweza kudhibiti vitendo vya udhibiti vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo ukatili wa kijinsia . Akitoa tathimini hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Tume za haki za binadamu Francisis Nzuki amesema kuwa kumekuwa na ufuatiliaji wa watuhumiwa wa naohusika katika vitendo vya ukatili wakijinsia hali inayochangiwa na kupungua kwa vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia japokuwa kumekuwapo na changamoto mbalimbali juu ya ufuatiliaji wa vitendo hivyo . ‘’Tumeweza kufuatilia na kutimiza malengo yamilenia 17 ambayo yanamgusa binadamu ikiwemo utoaji wa elimu kudhibiti vitendo vya ukatili wakijinsia na kusimamia usawa wa kijinsia katika Nyanja za maamuzi katika ngazi mbalimbali za kiserikali ‘’Alisema Mkurugenziwa haki za Binadamu Francisis Nzuki. Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Francisisi NZUKI alisema kuwa tume hiyo imeweza kupanua wigo wa upatikanaji wa haki hali inayochangiwa baadhi yavitendo vya ukikwaji wa haki za binadamu kuweza kupungua ikiwemo kufuatiliaji wavitendo vya ukiukwaji wa maadili katika sehemu za hospitali za umma . Alisema kuwa kumeweza kutolewa kwa semina elekezi kwa watendaj i wa afya baada ya kutoa semina elekezi nakutoa vipeperushi juu ya maadili ya mtumishi wa umma katika sekta hiyo juu ya kuwajali wagonjwa nakuto toa huduma ya afya kwa upendeleo hali inayo changiwa kupungungua kwavitendo vya ukiukwaji wa maadili katika sekta hiyo ya afya . ‘’Tumeweza kufuatilia malalamiko katika hospitali za mikoa na ukiukwaji wa maadili katika sekta ya afya nakutumia njia mbalimbali za kuelimisha juu ya ukiukwaji haki za binadamu ikiwemo kutoa vipeperushi ‘’Aliongeza NZUKI . MKUU Wa kitengo cha ushauri wa Haki za binadamu Kutoka Shirika la umoja wa mataifa Chitralekha Massy amesema kuwa kumekuwepo nachangamoto nyingi katika nchi zinazoendelea katika utekelezwaji wa haki za binadamu ikiwemo haki ya Kupata elimu chakula na afya hali inayopelekea nchi nyingi barani humo kuwanyuma juu ya utekelezwaji wa haki za binadamu . Alisema kuwa sambamba nachangamoto hizo kumekuwa na ubaguzi wa kijinsia katika kumiliki ardhi ambapo jamii za kutka afrika zimekuwa zikimnyanyasa mwanamke katika kumiliki wa wa ardhi . ‘’kumekuwa nachangamoto za kutokumilki rasmali kwa wanawake ikiwemo ardhi hii nikutokana na mila potofu kwa baadhi za mila zinazotoka katika bara la afrika ‘’Alisema chitralekha .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni