Jumanne, 10 Novemba 2015

NEC YATANGAZA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUTKANA NA VIFO VYA WAGOMBEA .


Timothy Marko.
TUME ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC)imetangaza tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi kwa majimbo yaliyokutwa na kasoro mbalimbali katika uchaguzi uliofanyika October 25 Mwaka huu ambapo tume hiyo imezitaja sababu zakurudiwa uchaguzi huo katika majimbo hayo nipamoja na kufariki kwa wagombea .

Akizungumza Katika Mkutano wa waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa sheria katika tume hiyo ya uchaguzi Emanueli Kavishe amesema kuwa uchaguzi huo unatarajia kufanyika Novemba 22 hadi Desemba 20 mwaka huu .

''Majimbo pamoja na kata zitakazo rudiwa uchaguzi nipamoja na Jimbo la lushoto mkoani Tanga, jimbo la ulanga Mashariki mkoani morogoro ambapo uchaguzi huo katika majimbo haya unatarajiwa kufanyika Novemba 22,majimbo mengine nipamoja na Mulebakatika halimashauri ya Muleba Kusini,Uyole Mbeya mjini,Bukene katika halimashauri ya shinyanga ,Msingi halimashuri ya Mkalama ,Boma Ng'ombe halimashauli ya Hai ,Kasulo halimashauri ya Ngara,pamoja na Halimashauri ya shinyanga Kata ya Bukene'' Alisema Emanuel Kawishe.

Mkurugenzi wa sheria Wa tume ya uchaguzi NEC Emanueli Kawishe alisema kuwa Majimbo mengine yatakayo rudiwa uchaguzi Desemba 13 mwaka huu nipamoja na Arusha Mjini mkoani ARUSHA ,Handeni mkoani Tanga, majimbo mengine ni Mvomero halimashauri ya Movemero .

Aidha Emanueli Kawishe alisema kuwa maeneo mengine ambayo yanatarajiwa kurudiwa uchaguzi wawabunge na madiwani Desemba20 mwaka huu nipamoja na jimbo la Ludewa mkoani Njombe,Masasi Mjini MKoani Mtwara. 

''Vituo vya kupigia kura ni vile vilivyotumika katika uchaguzi wa urais Octobar 25 vituo vyote vitafunguliwa saa moja asubuhi nakufungwa saa 10 jioni nawatakao ruhusiwa kupiga kura niwale walio na kadi za mpigakura na ambao wamo katika Daftari la

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni