Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Jumatatu, 23 Novemba 2015
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUSHIRIKIANA NA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI KUZUIA AJALI.
Timothy Marko.
JESHI lapolisi kikosi cha usalama Barabarani nchini kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani imeanzisha kampeni maalumu ya katika kudhibiti tabia hatarishi za madereva wa mabasi waoendao mikoani ilikudhititi ajali zinazotokea katika sikukuu za mwisho wamwaka .
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo,jijini Dar es salaam Kamishina wa polisi wakikosi cha usalama barabarani ACP Mohamed MPINGA amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa njia ya video pamoja na cd nakushirikiana na mabalozi hao katika utoaji wa elimu ya usalama barabani ikiwemo kuwataka abiria kutoa taarifa kwajeshi hilo pindi wanapohisi mwendokasi wadereva wa basi Hauridhishi .
‘’Sisi kama jeshi lapolisi kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani tumesha anza kutoa elimu kwa abiria wanaokwenda mikoani kuhakikisha wanakwenda salama kampeni hii ijulikanayo ‘’ paza sauti ‘’inalenga kukuza uelewa naufahamu haki nawajibu kwa abiria katika kutoa taarifa ‘’Alisema kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mohamed Mpinga .
Kamishina Mohamed Mpinga alisema kuwa ajari nyingi zinazotokea hapanchini zinatokana na makosa yakibinadamu yanayotokana kutokuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani nakuwa taka abiria kuto kaa kimya pindi wanapohisi kuzidi kwa mwendo kasi .
Alisema kuwa sambamba na kujipanga kudhibiti ajari za barabarani kwa kutoa elimu pia jeshi hilo limejipanga katika kutoa vibali mbalimbali vya kwenda mikoani ikiwemo kufanya ukaguzi wa gari husika kabla ya basi kufanya safari zake mikoani .
‘’KATIKA kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka tumejipanga katika kutoa vibali vya usafirishaji wa mabasi ya endayo mikoani kwa kufanya ukaguzi maalumu ilkuweza kudhibiti ajari zinazotoekea kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ‘’ Aliongeza Kamishina Mpinga .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni