Timothy Marko.
JESHI la polisi nchini limezuia maandamano ya Chama cha Demkrasia na maendeleo (Chadema )kufuatia chama hicho kushinikikiza kusititishwa kwa bunge la katiba linaloendelea huko mjini Dodoma kufuatia chama hicho kutofuata taratibu za kufanya maandamano .
Akizungumza jijini mapema hii leo,Kamishina wajeshi lapolisi operesheni na mafunzo Paulo Chagonja amesema kuwa kufuatia barua iliyotolewa September 14 mwaka huu na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kuwa yeye nanawafuasi wachama chake wanajipanga kufanya maandamano nchi nzima jeshi hilo limesema kuwa haitakubaliana nahatua hiyo nakusisitiza kuwa siasa zina mipaka yake nakua zinapokiukwa sheria na taratibu zake swalahilo nikosa lajinai na wala si siasa tena .
‘’Aidha ieleweke wazi kwamba siasa zina mipaka yake zinapo vuka mipaka hiyo nakuanza kwenda kinyume cha sheria kanuni na taratibu za nchi hiyo inageuka kuwa jinai nawala si siasa tena hivyo mtu yeyote atakaye tumia mwamvuri wa siasa nakutaka kuvuruga amani nautulivu uliopo hapa nchini jeshi lapolisi halito mvumilia nahalitosita kumchukulia hatua kali’’Alisema KAMISHINA Paulo Chagonja.
Kamishina CHAGONJA alisema kuwa kufuatia onyohilo jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kufuata utaratibu na kuzingatia sheria ilikuepuka kauli zittakazoleta uvunjifu wa sheria .
Katika hatua nyingine jeshi lapolisi kanda maalum jijini Dar es salaam linsawashikilia watu wawili ambao niwakazi wa magomeni BARAKA MZEE (34) NAASIB KULWA Kwakukutwa na tiketi bandia 424 zamechi yangao yahisani kati yanga na azam ambapo mchezo huo uliofanyikajana katika wauwaja wa taifa jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni