Timothy Marko
KUFUATIA
taarifa zilizo chapishwa hivi karibuni na gazeti moja hapa nchini kuwa
mkurugenzi wa Shirika la nyumba la taifa (NHC),Nehemia Mchechu kuwa ameundiwa
zengwe na bodi ya wakurugenzi wa shirika la NHC kuwa kiongozi washirika hilo
harudishwi kwenye wadhifa wake kama
kiongozi wa shirika hilo, Bodi ya wakurugenzi imekanusha kuhusiana na taarifa
hiyo .
Akizungumza na
waandishi wa Habari jijini leo ,Kaimu Mkurugenzi wa shirika lanyumba nchini
(NHC)David Shambwe, amesema kuwa bodi ya shirika hilo ina miezi miwili tu mara
baada yakuundwa nakusisitiza kuwa tangu bodi hiyo iundwe haijawahi kukaa kikao
chochote juu ya kumuondoa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo wala kupunguza
menejimenti iliyopo sasa ya shirika hilo.
‘’Kwanza
naomba ifahamike kuwa Bodi ya wakurugenzi ya NHCina miezi miwili tangu iteuliwe
na mamlaka husika na hajawahi kukaa katika kikao chochote kujadili kumuondoa
mkurugenzi mkuu na kupunguza menejimenti ya shirika iliyopo sasa’’Alisema David
Shambwe.
Shambwe
alisema kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Nehemia Mchechu bado wanamkataba
naye pamoja naMenejimenti ya shirika hilo hivyo hoja ya kuwa Mchechu ameundiwa
zengwe na Menejimenti ya shirika hilo la NHChaina ukweli wowote.
Alisema
kutokuwepo kwa mkurugenzi mkuu huyo kwenye ufunguzi wa miradi inayoendelea ya
shirika hilo hakutokani nakuundiwa mizengwe kama ilivyoripotiwa awali na gazeti
hilo.
‘’Bwana
mchechu alikuwa katika likizo ya mwaka iliyoanza tarehe 30 juni nakumalizika julai 18mwaka huu
likizo hii ni stahili halali kwa Bw.Mchechu kama ilivyo kwa watumishi waumma,na
haikua ni mizengwe ya kumondoa kama ilivyoripotiwa na gazeti hili mchechu yupo
kikazi nje ya nchi anatarajiwa kuwa ofisini kwake tarehe 28julai mwakahuu’’Aliongeza
David Shambwe .
Katika hatua
nyingine Naibu mkurugenzi washirika hilo aliviomba vyombo vya habari hapa
nchini kuendelea kutoa habari zenye usahihi na ukweli ilikuweza kuwafahamisha
wananchi ikiwa vyombo hivyo vina dhamana kubwa katika taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni