Timothy Marko.
MKAZI wa Sinza Madukani, Filimon Joel (28), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kanga
aliyokuwa ameifunga kwenye dari la chumba chake alichokuwa akiishi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema, tukio hilo lilitokea juzi saa Sita mchana,chanzo na sababu za kujinyonga hazijafahamika, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili.
Katika tukio lingine Cristastus Kazimoto(23), mkazi wa Mbande ambaye ni dereva wa Pikipiki yenye namba ya usajili T.662 CJB Boxer, amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Musae Mumue (23), mkazi wa Msongola aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T.978 CNG Skymark akitokea Mbande kuelekea Chamanzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipoli Temeke,Engliberth Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, juzi saa 3:40 asubuhi huko Chamanzi.
Alisema wakati dereva Mumue akitokea Mbande kuelekea Chamanzi alihama kutoka upande wake wa kushoto na kwenda kulia na hatimaye kugongana.
Aliongeza kusema kuwa baada ya ajali hiyo pikipiki nyingine yenye namba za usajili T.828 CUX Fekon ikiendeshwa na Warioba Mbechi ilizigonga pikipiki hizo mbili ambazo tayari zilikwishapata ajali.
Kwa mujibu wa Kiondo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Temeke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni