Ijumaa, 4 Julai 2014

AMREF LAJIKITA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA ZA MAMA NAMTOTO.

Timothy  Marko.
KATIKA  kuboresha huduma za afya natiba hapa nchini Shirika lisilo la kiserikali  Amref Health Africa  Tanzania limesema kuwa ilikuweza kupanua wigo wahuduma zake ikiwemo kufanya utafiti mbalimbali inayohusu kuboresha hali mama namtoto pamoja nakufanya utafiti wamagonjwa mbalimbali  ikiwemo  ugonjwa wa ukimwi,  kifua kikuu , pamoja na maralia , shirika hilo limezindua nembo maalumu  ikuweza kuwafikia walengwa kama ilivyo jiwekea mikakati yake yakupanua huduma zake.
Akizungumza jijini leo  Mkurugenzi wa shirika hilo lisilo la kiserikali la Amref DK.Fetus ilako amesema kuwa uzindunduzi wa nembo hiyo mpya unaendana sambamba na uimarishaji wa utoaji huduma za afya pamoja nakutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo kuanzisha miradi mbalimbali ya afya ya mama na mtoto na ile ihusuyo magonjwa mbalimbali kama vile ukimwi ,kifua kikuu pamoja na  maralia .
‘’Uzinduzi huu wa nembo mpya umekuja ilikuendana na majukumu yetu ya sasa ambayo yamekuwa ni zaidi ya utafiti na utoaji huduma za tiba ,kwasasa tunajikita katika uimarishaji wa mifumo yautoaji huduma namiradi mbalimbali ya afya ikiwemo afya yamama namtoto ,kifua kikuu ,ukimwi na malaria  ikijumuhisha timu malumu ya madakitari bingwa’’Alisema DK fetus ilako .
DK ilako alisema kufuatana na uzinduzi wa nembo yetu mpya hautoweza kuathiri kiwango kinachotolewa na shirika hilo katika kutoa huduma za afya nazile zinazo husiana na maswala ya utafiti wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi.
Alisema dhamira ya shilika hilo nikuahakikisha kuwa afya bora inapatikana hususan nchi zilizo katika ukanda wa bara la afrika ilikuweza kuwa na afya endelevu katika kushirikiana na jamii katika kuibua nakupanga mipango mbalimbali .
‘’Tunaamini kuwa kuwa nembo yetu mpya inaonesha uwepo wa Amref Health Africa  kimataifa na kuendeleza mipango na utendaji kazi  na kufikia malengo kama ilivyokusudiwa ‘’Alisema Fetus ilako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni