Jumanne, 20 Mei 2014

JESHI LAPOLISI YA ENDELEA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KUHUSIANA NA KIFO CHA MENEJA WA BIASHARA WA EWURA

Timothy  Marko.
Jeshi kanda maalum  jijijini  Dar es  salaam limeanza kufanya uchunguzi wa kina  kufuatia  kifo  cha aliyekuwa meneja  wabiashara  wa mamlaka ya udhibiti wa maji nanishati (EWURA) Julius  Gashagaza (51) ambapo afisa huyo alikutwa amefariki  katika  meneo ya  yombo vituka katika nyumba yakulala wageni  itwayo Mwanga lodge.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini ,kamishina wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema katika uchunguzi wa awali ulionyeshakuwa afisa huyo wa ewura alikuwa katika nyumba yakulala katika chumba namba 133akiwa katika hali inayoashiria kujinyonga kwa kutumia tai aliyokuwa ameivaa mwenyewe.
‘’katika hali isiyo yakawaida jeshi letu tulifanya uchunguzi wa awali tuli pata taarifa kuwa afisa huyo alikuwa amekutwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo mwanga lodge akiwa amejinyonga kwa kutumia tai aliyokuwa ameivaa mwenyewe ‘’alisema kamanda Suileiman Kova.
Kamanda suileman kova alisema kuwa licha yajeshi la polisi kupata maelezo hayo bado jeshi lake linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ilkuondoa utata ulioanza kujitokeza baada ya kuzagaa taarifa ambazo sio rasmi kueleza kuwa kifo chake kilitokea kufuatia kutoelewana na viongozi wenzake kuhusiana na maswala yakikazi.
Alisema kuwa kinachofanywa najeshi hilo ni kupata maelezo kuhusiana na mwenendo washughuli za marehemu na hali iliyo msibu kabla yakifo chake kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote wa mdomo wala maandishi.
‘’kinacho fanyika sasa ni kupata maelezo ya kina kuhusiana na mwenendo wa shughuli za marehemu na hali iliyomsibu kabla yakifo chake kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote aidha wamaandishi wala mdomo’’aliongeza kamanda Suileman kova.
Katika hatua nyingine jeshi lapolisi kandamaalum limewa kamata majambazi wawili wakiwa nabastola moja aina ya star huko kiwalani jijini Dar es salaam yenye namba za usajili SACAL22LR HK708022 ikiwa na risasi moja ambapo walipo hojiwa majambazi hao walikiri kuhusika natukio hilo.
‘’majambazi tulio wakamata nipamoja ALLY Likwale ,na Charles malima (32)aidha watuhumiwa hawa wanasakwa kwambinu zote ilikuwafikisha mahakamani ilihatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao’’aliongeza kova.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni